Pages

Sunday, December 14, 2014

Sifanyi Filamu Kusaka Umaarufu Bali Kumtumikia Mungu: Sallai Majasiri

Sallai
Sallai Majasiri sio jina geni hasa kwa waafrika waishio nchi za Scandinavia ambao hujishughulisha na sanaa mbalimbali.
Hata hivyo yeye yupo katika sanaa ya kumtumikia Mungu zaidi yaani upande wa nyimbo za gospel na filamu zinazohusu kumtumikia Mungu na kuachana na maovu. Sallai sio jina gani kwani habari zake zimekuwa zikitokea hata hapa, hivyo baada ya kimya kidogo SWP ilipata nafasi ya kuzungumza nae machache hivi karibuni kama ifuatavyo.

SWP: Tumesikia ulikuwa kimya kidogo kwa ajli ya mambo ya ofisi yako ya sanaa, je unaweza kuwaambia mashabiki wa kazi zako ukimya huo ulikuwa wa nini hasa?

SALLAI: Nilikuwa kimya sana kwa haya mambo ya filamu maana siko huko kibiashara au matangazo ila tu kwangu nimeingia katika filamu kuhubiri neno la MUNGU alie hai, kuwaambia wanadamu wenzangu kuwa WATUBU dhambi na kumkimbilia YESU KRISTO, maana anakuja upesi kulichukua kanisa lake ambalo ni mtu yule alie jikana na kujitenga na mambo ya dunia ... Halafu mimi sipendelei kuita wenzangu eti mashabiki maana mimi sitafuti umaarufu na wala siko bali KRISTO ndani yangu Yeye ni maarufu kuliko neno lenyewe maarufu .

SWP: Vipi unaweza kuelezea uhusika(character) yako katika filamu mpya ya Sorry My Wife?

SALLAI: )Uhusika wangu katika filamu mpya ya Sorry My Wife chini ya VAD FILM PRODUCTIONS yenye makazi yake kule nchini Denmark, nilihusika kama Mchungaji aliyekuwa akiwafariji na kuwaombea watu hata kuunganisha ndoa zenye matatizo kwa uwezo wa MUNGU.

SWP: Nini unakikimbuka au kukifurahia wakati mliokuwa mnashuti Sorry My Wife?

SALLAI: Hahahah !.... Trim mimi siyo msemaji wa kundi la VAD Film Productions.... Kuna vingi sana ninavyokumbuka wakati tulivyokuwa tukishuti filamu hiyo ya Sorry My Wife, kama namna wanavyoshuti kwa ustadi mzuri na umakini wa msimamizi wao Jay na Rais Safari na Zawadi. Nakumbuka wakati mzuri sana niliogawa nao kwa muda mchahe ule ambao tulikaa pamoja na kuwa kama vile tumeishi kwa miaka mingi pamoja. Vichekesho vya Selembe na Dada Lucy Komba na Richard bila kumsahau dada Safi . Hakika wana ushirikiano mzuri sana nawaombea MUNGU wafike mbali na wahubiri injili kupitia filamu zao wakiwausia watu waache dhambi na kumrudia MUNGU ili wasije siku ile ya hukumu wakadaiwa na damu za watu .
Akiwa na Rehema Nkalami mtangazaji wa Swahili Talk Radio Denmark

SWP; Unajihusha na muziki wa injili ukiachilia mbali filamu hasa za kumtukuza Mungu, je watoto wako kuna anayefuata nyayo zako?

SALLAI: Ndiyo awali nilijihusisha sana na muziki wa injili lakini sasa nimeona wito wangu upo zaidi kwenye filamu za Injili . Wanangu wote ni watumishi wa MUNGU wanaigiza na kuimba sifa za MUNGU kama mfalme Daudi. Nani jukumu langu kila saa kumlilia MUNGU kwa ajili yao wanangu pamoja na watoto wa ndugu zangu hata marafiki na watoto wote ulimwenguni kuwa MUNGU awajaze Roho yake na kuwatenganisha na dunia hii, nia na shauku na tamaa zao zote ziwe kwa YESU KRISTO tu siku zao zote. AMEN !

SWP: Kwasasa watu wategemee nini i toka Majasiri Productions?

SALLAI: Wategemee kuongeleshwa na MUNGU Muumba kupitia kazi zetu za Majasiri, kadri jinsi Roho wa MUNGU atazungumza na sisi ndiyo nasi tutazidi kuachia kazi zetu ambazo nia na madhuni yetu ni moja tu, kuliandaa kanisa la Kristo kwa ajili ya UNYAKUZI . Kuwaambia watu umuhimu wa kanisa kujitenga na mambo ya dunia hii . Kanisa la MUNGU halitaki kabisa kufanana au kuenenda kwa namna ya dunia hii.... Maana Uzima wa milele ni bora sana kuliko vitu vyote vya dunia hii, ndiyo maana Majasiri hatuko kibiashara hatufanyi film za biashara au kuusaka umaarufu maana vyote ni ubatili na haviwezi kumsadia mtu mbele ya hukumu ya MUNGU bali tu usafi wa roho katika KRISTO YESU ambae ndiye uzima mwenyewe .

Tumewaona wengi ambao walikuwa na umaarufu mkuu na uwezo wa kipesa lakini waliishia vibaya sana na kupotelea dhambini. Hapa duniani ndiyo mahala pekee ambapo mwanadamu anaweza kuuandaa uzima wake wa milele kwa ajili ya Ahera au Jehanamu . Mbingu haiji kwa bahati bali kwa nguvu nyngi mno, ambayo ndiyo kuyakataa maovu dhambi za ulevi uzinzi, ushoga, uozo wa tabia,Chuki, uchawi na tamaa zote mbaya za dunia hii . Twahitaji kumuabudu MUNGU katika roho na kweli ,hata mwili wetu kama hekalu la MUNGU la paswa kumtukuza MUNGU kwa yote.... Kwahiyo watu wategemee mambo kama haya katika kazi za Majasiri Productions, Na haya yote twayaweza katika Bwana atuwezeshae!
mdogo wake aitwae Gilbert akiwa location katika moja ya short film yao

SWP: Una matarajio yoyote ya kufanya kazi na wasanii wa gospel wa kiafrika? je ni nani?

SALLAI: Kwasasa tuko kimya na tunafanya kazi na kujiweka sawa sana sana kiroho, tukimtafuta Roho wa MUNGU zaidi ya yote, mpango huo wa kushirikisha wengine upo na tuna mawasiliano na wengi sana, ila tu ni wale ambao maono yetu yanafanana ... Kila mara tutakuja kwa surprise kazi ziko ila hatuna pupa bali tunataka kuwa makini sana . Na hivi karibuni tutaachia kazi ya kwanza kabisa ya Majasiri .

SWP: Chochote ambacho ungependa kugusia kwa wanaofuatilia kazi zako?

SALLAI: Ninatoa mualiko kwa wote ambao wangepanda tujifunze pamoja kwa KRISTO YESU wakuje twitter na facebook :
Majasiri Productions, Hapo watakuatana na waalimu watu wa MUNGU wanaojitolea kila siku ndani ya hiyo page kwa ajili ya utukufu wa MUNGU wakitarajia taji kuu mbinguni siku za hivi karibuni nitawaweka wazi . MUNGU awabariki sana.

No comments:

Post a Comment