Pages

Friday, December 12, 2014

Ni Kubebeshana Mizigo Kulazimisha Watu Michango Ya Harusi: Ray

Actor maarufu Tanzania Ray Vicent Kigosi amesema kuwa hapendi mambo ya michango ya harusi hasa kwa watu wenye uwezo kwa madai ni usumbufu kwa wengine.
Akizungumza katika kipindi cha Boys Boys katika TV1 Ray alisema hata anapokutana na mesage za michango ya harusi huwa ngumu kupokea simu

"Sio mtu unawapa watu mizigo isiyo ya kwao, Kama una uwezo fanya mwenyewe, kwa sababu katika maisha tunaambiwa kuna vitu vitatu, kuzaliwa, harusi na mwisho kifo! Sasa kama una uwezo, fanya kitu kikubwa zaidi katika maisha yako, lakini sio michango nikikutana na meseji ya mchango, hata kupokea simu inakuwa shida," alisema Ray

No comments:

Post a Comment