Pages

Sunday, December 7, 2014

Mafundi Wapigwa Na Kuvuliwa Nguo Kubaki Uchi Nyumbani Kwa Wema Sepetu.

Wema Sepetu ameingia katika skendo ambayo inaweza kumshushia hadhi yake !.....Mtandao wa Bongo5 umeripoti kuwa mafundi ambao huenda nyumbani kwa Wema Sepetu mara kwa mara kumkarabatia nyumba yake wanadaiwa kupigwa na kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo nyumbani kwa Wema Sepetu kwa madai ya upotevu wa simu huku Wema mwenyewe akiwepo.


Jirani mmoja kwa jina la Mama Steve akizungumza na Bongo5 jana alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa hii majira ya saa 5 asubuhi mpaka saa 9 jioni.

"Waliopigwa na kulazwa chini uchi wa mnyama ni mafundi ambao wanakujaga kila siku kumtengenezea nyumba yake, sasa baada ya kumaliza kazi yao wakaondoka, baada ya kuondoka wakaitwa tena na kuambiwa kuna simu imeibiwa ndani ndo mtiti ukaanza" alisema jirani huyo Mama Steve

"Petit Man(mfanyakazi wa Wema) akatumwa kuchukua mabaunsa 7 na baada ya kufika wakapandisha muziki hadi mwisho ili sisi tusisikie nini kinaendelea huko ndani, sasa kulikuwa kuna mtu alikuwa anapita hapa kwenye geti lao akasikia kuna mtu analia sana, ikambidi akachungulie ndo akawakuta mafundi wawili wamelezwa chini uchi wa mnyama wanapigwa na hawana nguvu kabisa !. ndo yule jamaa kwakuwa anamjua yule fundi akaita watu wakaanza kugonga geti ili wafumgue geti lakini hawakufungua geti, tukawa tunasikia sauti ya Wema "jamani waacheni hao mtawauwaa" lakini anasema hivyo wakati yeye anaonyesha ndio alikuwa kinara wa matukio hayo, Wema ana roho ya kikatili sana, amefanya matukio mengi lakini hilo hapana ! yaani kama anataka usalama wake anatakiwa ahame vinginevyo vijana watamfanyia tukio la kinyama sana" aliongeza mama huyo

"Baada ya watu kuwa wengi sana pale nje ndo geti likafunguliwa watu wakaingia kuwachukua wale vijana wakiwa hawajitambui na wapo uchi ndo wakapelekwa hospitali, sasa baada ya kupelekwa hospitali polisi wa kituo cha mabatini  na wao wakagonga geti wakawa hawataki kulifungua polisi wakapindukia na kuingia kuwakamata baadhi ya watu na kuondoka nao, hilo ndo tukio alilolifanya mwandada wenu ambaye anadai alikuwa Miss Tanzania" alisema Mama Steve

Baada ya tukio hilo Mjumbe wa Nyumba kumi aliyejulikana kwa jina la Mwarami alitafutwa na Bongo5 kuulizwa kuhusu tukio hilo, alikubali tukio hilo kutokea lakini alisema ahatatoa ufafanuzi zaidi kwakuwa tayari limefikishwa polisi kituo cha Mabatini. Bongo5 walipoenda kituoni hapo waliambiwa wamuone mkuu wa kituo ambaye hata hivyo hakuwepo kwa muda huo.

Petit Man ambaye yupo karibu na Wema Sepetu alipoulizwa na Bongo5 kuhusu tukio hilo alisema ni kweli mafundi hao walipigwa nyumbani kwa Wema lakini alikana kuwa walivuliwa nguo na kubaki uchi wa mnyama "Yeah kuna tukio lilitokea lakini hakuna mtu aliyevuliwa nguo" alisema Petit Man kisha akakata simu

Tukio hilo la kiudhalilishaji hata kama mafundi kweli waliiba simu lakini linaweza kumshusha Wema Sepetu hasa kwa mashabiki wake

No comments:

Post a Comment