Pages

Friday, December 19, 2014

Kampuni Ya Steps Entertainment Yatangaza Kushusha Bei Ya Filamu Zake Kupambana Na Maharamia.

Kampuni ya Steps Entertainment Tanzania ambayo ni moja ya kampuni zinazosambaza filamu za kitanzania leo imetangaza kuwa kuanzia mwezi February 2015 itaanza kuuza filamu zake kwa bei ya shilingi 1500 za kitanzania badala ya 3000 kama bei ya rejereja.
Steps walizungumza hayo katika ukumbi wa Habari Maelezo katika mkutano na waandishi wa habari huku baadhi ya wasanii ambao kazi zao husambazwa na kampuni hiyo wakiwepo.

Steps imesema imechukua hatua hiyo kama sehemu ya kupambana na maharamia wa kazi za wasanii ambao wanafanya kazi hiyo bila kificho na serikali ikionekana kama kushindwa kuwadhibiti.

Nini mtazamo wako juu ya hili..?

No comments:

Post a Comment