Pages

Monday, December 15, 2014

Diamond Platnumz Kudaiwa Kutudhalilisha Ni Uongo Uliopikwa: Susumila

Susumila
Susumila msanii wa Kenya amekana taarifa zilizoenea kuwa yeye na Nyota Ndogo walidhalilishwa na Diamond Platnumz na organizer wa show yake huko Mombasa nchini Kenya hivi juzi. Mtandao wa Standard media wa kenya umeaandika habari hizo soma HAPA kama hukusoma.
Katika habari hiyo ilidaiwa Diamond hakutaka kukaa pamoja na kina Nyota Ndogo kwenye VIP Lounge aliyopngiwa na wasanii wengine ambao walikuwa watumbuize akiwemo Nyota Ndogo huku ikidaiwa walinyimwa maji ya chupa kwa madai yalikuwa kwa ajili ya Diamond na crew yake pekee hivyo Kina Susumila na Nyota Ndogo wakanywe maji ya Bomba

Hata hivyo Susumila ambaye ni msanii anayedaiwa kudhalilishwa amekana madai hayo kuwa ni ya uongo na kupikwa wakati akizungumza na mtangazaji Willy M Tuva katika Kipindi cha Mambo Mseto, Radio Citezen,
"Hizo story ni za uongo, sidhani kama Diamond anaweza kufanya hivyo au ana haki ya kufanya hivyo, kama nimekuwa mistreated labda niwe mistreared na yule mtu aliyenipatia show, sio Diamond kwasababu na yeye ameitwa kwenye show kama mimi" alisema msanii huyo

Na kuongeza "unajua Mombasa wanapenda vitu vya uongo, hakuna mtu ana-complain kuhusu show kuwa ilikuwa mbovu ama nini, watu wanatafuta vijisababu vidogovidogo wanasema sijui nimenyimwa maji, mimi nilipanda steji nikiwa na chupa yangu ikiwa kwa DJ , nika-perform dancers wangu walipokuwa wanafanya set yao nikachukuwa maji nikanywa pale pale, kwa DJ kulikuwa na chupa kama kumi za maji hazijafunguliwa. Sijui story ilianzia wapi lakini kufikia kwenye saa tatu, saa nne ilikuwa kwenye blogs karibia zote za huku(Mombasa)"

No comments:

Post a Comment