Pages

Friday, December 5, 2014

Aunty Ezekiel Mjamzito Wa Miezi 4, Wema Sepetu Amsindikiza Clinic

Picha ya Aunty akiwa na Wema iliyopigwa wiki ilopita ikimuonyesha Aunty akiwa na kitumbo
Aunty Ezekiel andaiwa tena kuwa mjamzito licha ya kukanusha mwezi October mwaka huu katika birthday yake.
Safari hii tena Aunty anadaiwa kuwa mjamzito wa miezi 4 kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu nae kilipozungumza na Globalpublishers. Rafiki yake wa karibu Wema Sepetu anadaiwa kumsindikiza Clinic "Mimi najua muda mrefu na jinsi anavyoonekana kwa sasa hakuna ubishi kwani ujauzito wake una kama miezi minne hivi" kilisema chanzo hicho

Aunty kama kweli ni mjamzito basi mimba yake itakuwa kaipata nje ya ndoa kwa mujibu wa gossip mongers kwasabau hajakutana na mumewe muda mrefu ambapo anadaiwa kuwa gerezani huko Dubai. Mhusika wa mimba hiyo anadaiwa kuwa dancer wa Diamond Platnumz aitwaye Moze Iyobo.

Hata hivyo Aunty alipoulizwa tena na Globalpublishers alikanusha kwa kusema "Sina huo ujauzito, labda ni kwa sababu ya aina ya magauni ninayovaa"

No comments:

Post a Comment