Pages

Thursday, November 20, 2014

Zari Ni Shoga'ngu Wa Kitambo Hana Uhusiano Wa Kimapenzi Na Diamond: Wema Sepetu

Wema na Diamond
Wema Sepetu amesema kuwa Zari The Boss Lady ni rafiki yake wa siku nyingi na wala hana uhusiano na Diamond Platnumz kama inavyozushwa bali wanafanya project flani pamoja.
Akizungumza na Globalpublishers Wema amesema kuwa amempa likizo kwanza Diamond ili kila mmoja afanya mambo yake kwa uhuru bila kufafanua zaidi kama wameachana kabisa au likizo hiyo ni ya muda gani, ingawa inadaiwa miezi michache nyuma Diamond aliposema hana mpango wa kuoa hivi karibuni Wema alichefuka na kauli hiyo.

"Kwanza naomba watu wajue kuwa, projekti ya Diamond na Zari ninaijua na bahati nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Diamond siku nyingi" alisema Wema

Kwa upande wa Diamond alipoulizwa na Globalpublishers alisema

"Dah! Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya kisiasa tu.
ashindwa kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.
“Mimi nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee"
Hata hivyo Diamond na Wema wamekuwa na tabia ya kuachana na kurudiana rejareja hivyo kuna uwezekano wakarudiana tena muda si mrefu. Vile vile Wema amesema Zari ni shoga'ke wa kitambo lakini historia inaonyesha mashoga zake wa karibu walishamzunguka kwa kumkwapulia mpenzi aidha Diamond au mwingine.

No comments:

Post a Comment