Pages

Sunday, November 9, 2014

Shamsa Ford Na Rammy Galis Wanakuja Na Muendelezo Wa Filamu Ya Chausiku.

Shamsa Ford
Muendelezo wa filamu ya Chausiku ambayo imetokea kupendwa sana na mashabiki tangu ilipotoka mwezi uliopita unakuja. Kwa mujibu wa waandaji wa filamu hiyo wataanza kutengenezan filamu hiyo hivi karibuni.
Chausiki imechezwa na Shamsa Ford kama msichana mshari na muongeaji sana toka maeneo ya uswalini mjini akiwa amependwa na mvulana msomi Rammy Galis toka familia ya kitajiri lakini vituko vyake na uongeaji mwingi unawatibua wazazi wa mwanaume baada ya kwenda kumtambulisha kama mpenzi wake.

Pia wamo Mayasa Mrisho, Cathy Rupia na Annasiri Msangi. Kwa mujibu wa waandaaji hao muendelezo wa filamu hiyo utakuwa tofauti na iliyopita lakini ladha ikiwa kubwa kumburudisha na kumfundisha mtazamaji.


No comments:

Post a Comment