Pages

Wednesday, November 26, 2014

Irene Uwoya Na Jaguar Wa Kenya Wakiri Kuwa Wapenzi, Maandalizi Ya Ndoa Yaanza.

Miezi takribani mitano iliyopita Swahiliworldplanet ilipata habari toka chanzo kimoja nchini Kenya kuwa kiliwaona  star wa filamu Tanzania Irene Uwoya na mwanamuziki wa Kenya Jaguar katika hotel moja  Nairobi wakiwa kimahaba lakini kwa tahadhari flani.
Soma habari hiyo hapa Uwoya Na Jaguar Wakutana Kenya. Sasa habari za wawili hao kuwa wapenzi zimeanza kuwa kweupe baada ya Jaguar kusema kuwa soon anakuja Tanzania kumuona Uwoya na kuwaona wazazi wake issue ikionekana ni kujitambulisha na kutoa posa ili kumuoa Uwoya mmoja wa mastaa wenye mvuto Tanzania. Akizungumza na E-Newz ya East African Television, Jaguar alisem kuwa anamkubali sana Uwoya

"mimi naona nitue Tanzania, sijue nije December, sijui nimjie Irene Uwoya, nije kumchukua, mwambie naja kumchukua, amenambia nione wazazi wake kwanza, naja December kumchukua" alisema Jagura aliyehit na wimbo wa Kigeugeu

 Bongo5 ilipomuuliza Uwoya kama anafahamu ujio wa Jaguar star huyo alikiri kuufahamu na kuonyesha furaha flani na kusema anakuja kufanya mipango ya kumuoa
"tuna mpango wa kuoana bado anakuja" alisema Uwoya ambaye aliwahi kufunga ndoa ya kifahari na msakata kambumbu wa Rwanda Hamad Ndikumana Katauti kabla ya ndoa yao kupigwa na vurumai la misukosuko ya kila aina.

No comments:

Post a Comment