Pages

Wednesday, November 19, 2014

Feza Kessy, Uti Warudishwa Big Brother Africa HotShot Kuwania $300,000

Feza
Katika hali ya kushangaza washiriki 10 wa mashindano yaliyopita ya Big Brother Africa wamerudishwa akiwemo mtanzania Feza kessy, Uti wa Nigeria, Elikem na wengineo.
Washiriki hao kwa mujibu wa Biggie pia wamekuwa sehemu ya Hotshot na hivyo kuwania dola $300,000 pamoja na washiriki wa mwaka huu. Kwa maana hiyo baada ya Laveda kutoka Tanzania kwasasa inawakilishwa na Idris na Feza.

Hata hivyo wengine wana wasiwasi kuwa wahiriki hao kumi wa awali wanaweza kutoka Jumapili hii ingawa kupitia Twitter account yao BBA waliandika wanashindana na wa sasa.

No comments:

Post a Comment