Pages

Sunday, October 26, 2014

Timoth Conrad Akumbana Na Ubaguzi Wa Rangi Nchini Marekani.

Tico akiwa ndani ya supermarket hiyo
Timoth Conrad amekumbana na ubaguzi wa rangi nchini Marekani aliko sasa kwa issue ndogo tu, akizungumza na Swahiliworldplanet tokea nchini humo alisema issue hiyo ilitokea katka supermarket moja ....


"Almanusura nishitakiwe hapa U.S.A kisa Nilikuwa supermarket ya Walmart, kuna mzungu mmoja alikuwa akichaguwa vitu vyake kwa manunuzi, sasa nikasimama pembeni yake kwa bahati mbaya aliponyanyuka akaajigonga ubavuni kwangu akapepesuka akaanguka, dah aliponyanyuka akaanza kupiga kelele na kuanza kutukana na kusema nimemuangusha kwa kumpiga teke... Mtu mzima nikapaniki katika kujitetea na kubisha sababu kajigonga mwenyewe.. basi kumbe hilo ni kosa... Huku mtu mweusi hana haki kumzidi mzungu hivyo mwanamke akataka kupiga simu polisi.
Watu wakamsihi akiwemo baba yangu na kusema kuwa ilikuwa ni bahati mbaya na akaomba msamaha badala yangu.. Dah ila nimejifunza kuwa hawa jamaa ni wabinafsi sana hawana utu kabisa... hata kusalimia hawawezi yaani kila mtu na vyake na lake" alisema Tico ambaye filamu yake ya Dogo Masai imeshinda Silicon Valley African Film Festival best african feature film. Waafrika wengi bado wamekuwa wakikumbana na suala la ubaguzi wa rangi katika nchi nyingi za Ulaya, Marekani na Asia

Tico akiwa nje ya supermarket hiyo


No comments:

Post a Comment