Pages

Wednesday, September 24, 2014

Nakerwa Na Kusikitishwa Sana Na Unyanyasaji Wa Wanawake: Nisha


Nisha akiwa na watoto yatima wa kituo cha Vingunguti
"Takribani week 2 au 3 nimesoma wanawake wachache walopigwa na waume zao,wapo waliokatwa viungo,kuchomwa moto n.k,

Baada ya matukio mengi ya ajabu yanayofanana na haya ndio inakuwa chanzo cha familia kutengana, chanzo cha watoto wengi wa mitaani,uhuni,magonjwa hatarishi n.k
Kuna wanaoripotiwa kunyanyasa wasichana wao wa kazi/Watoto wasio wao kwa mfano,huyu mwanamke (namuhifadhi jina sheria hainiruhusu) aliyekamatwa kwa kosa la kumuunguza pasi house girl wake kisa yeye hazai,mimi nimelelewa na mama wa kambo, ila mapenzi aliyonipa kumtoa moyoni siwezi na ndio maana napenda watoto wote.
Wanawake wenzangu tujiulize chanzo cha haya yote ni nini? Wanaume jamani kama una mawazo au mtu anakusumbua ni bora ukae naye chini muyazungumze, hakusikilizi sikio la kufa umuache aende kwao,
Na wewe mwanamke unayemnyanyasa mtoto wa mwanamke mwenzio acha sasa kama una mawazo au stress ni bora kutafuta daktari ili akutibu hakuna ambacho hakiwezekani,ukishindwa nitafute..na sisi wanawake tujitulize na kuwatii waume zetu kwa maana hata vitabu vya dini vimesisitiza hayo,vioo wenzangu vya jamii,hembu tuoneshe taswira ama mwangaza katika kuwatetea/kuelimisha mengi yanayotatiza jamii yetu- "tubadilikeni." amesema star mkubwa wa filamu nchini Nisha Salma Jabu ambapo kwa muda sasa amekuwa mstari wa mbele katika kuisadia jamii yenye matatizo mbalimbali wakiwemo yatima.



Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.


2 comments:

  1. MAANDISHI ULIYO YAANDIKA YANAUJUMBE MZITO AMBAO UKIZINGATIWA TATIZO LA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU LITAPUNGUA KAMA SIO KUISHA KABISA HONGERA KWAKO KWA UJUMBE MZITO WENYEMAANA HAPA UMEONYESHA MAANA YA KIOO CHA MSANII TENA KIOO SAFI KINACHO FUNDISHA MEMA MUNGU AKUJALIE NA AKUBARIKI KWA KILA JAMBO JEMA

    ReplyDelete
  2. Umegusa kundi muhimu sana kwenye jamii ingawa ndo kundi linaloingozwa kwa kunyanyaswa, Mungu akutie nguvu Nisha uzidi kuwa kioo na mfano bora kwa jamii yako, pia so mbaya kama utaanzisha kampeni juu ya kupinga hili, be blessed dear

    ReplyDelete