Thursday, September 18, 2014

Lulu, Linah Sanga Na Mama Kanumba Kuingia Sokoni Na Filamu Ya Mapenzi Ya Mungu.

Actress Maarufu nchini Lulu Elizabeth Michael, mwanamuziki Linah Sanga na Florah mTegoa ambaye ni mama Kanumba wanatarajiwa kuonekana katika filamu mpya inayoitwa Mapenzi Ya Mungu ambayo ilishutiwa baada ya Lulu kutoka Segerea na hapa tulikuwekea behind the scenes za filamu hiyo miezi kadhaa huko nyuma.
Filamu hiyo itakayosambazwa na Proin Promotions itaingia sokoni hivi karibuni.

 Kwasasa Lulu ambaye umaarufu wake ni mkubwa hutoa filamu chache kwa mwaka chini ya kampuni ya Proin Promotions.

No comments:

Post a Comment