Pages

Saturday, September 13, 2014

Kauli Ya Mh.Samweli Sita Yawachefua Wadau Wa Filamu Nchini, Wamtaka Awaombe Radhi.

Mh.Samweli Sita
Samweli Sita aliye mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba jana aliwafananisha UKAWA na wagizaji wa filamu nchini kwa madai ni "waigizaji" yaani ikiimaanisha aidha upeo wao ni mdogo au hawaeleweki.
Kauli yake hiyo imewachefua wadau wengi wa tasnia ya filamu nchini kwa madai kuwa alichosema Mh.Sita kinaonyesha waziwazi yeye kama mwenyekiti hawapi uzito mkubwa wasanii nchini ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipigania tasnia hiyo kuwa sector rasmi nchini bila mafanikio na kuishia kutumiwa katika kampeni za CCM anayotoka Sita wakati wa chaguzi mbalimbali. Mmoja wa waliochefuliwa na kauli hiyo ni Cameraman maarufu nchini Malik Nyumba ambaye alisema

"Waigizaji wamedhalilishwa na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Samweli Sita awewaita UKAWA hawana utofauti na waigizaji wa bongo movie huu mfano una maana gani? Ni kwamba waigizaji hawana upeo mkubwa wa kufikiri, UKAWA ni watu wa kufanya migomo ambayo kwa upande wao wako sawa ila kwa CCM ni uzembe, sasa je Bongo movie ni wazembe? Haya ni matusi ambayo Samweli Sita anatakiwa awatake radhi wadau wa bongo muvie. Pia kuna wanachama wa CCM kwenye Bongo muvie je haoni anawafedhehesha wana chama chao? Watajisikiaje 
anavyowaitaita hivyo?"

Sita alinukuliwa na media akisema "“Ni waigizaji wazuri sana. Hebu fikirieni vituko vyao. Tulipokuwa hapa mwanzoni tumevutana siku 18 kuhusu kura ya wazi ama ya siri. siku ya kuzikubali kanuni watu hawa waliopigania kura za siri kufa na kupona wakapiga kura za wazi"

Malik Nyumba

1 comment:

  1. Walalamikaj hawana akili km mlalamikiwaj,

    ReplyDelete