Pages

Wednesday, June 11, 2014

Sitaki Kusifiwa Nikifariki Kama Sifa Za Kazi Zangu Ninazo Basi Mnisifie Bado Nikiwa Hai: Riyama Ally

Riyama
Star wa filamu Swahiliwood Riyama Ally amewazodoa kimtindo baadhi ya wasanii wenzake wenye tabia za kumsifia mtu anapokufa badala ya kumpa sifa yake bado akiwa hai. Akizungumza na gazeti la Mwanasport Riyama amesema kuwa akifa hataki asifiwe kwakuwa haitakuwa na maana kwake kwa hiyo kama anastahili kupewa sifa kwa kazi zake za filamu basi apewe sasa "nasema mapema sitaki kusifiwa nikiwa nimefariki dunia, sifa mtu uipate ukiwa hai kama ni faida au kufurahia mwenyewe ujionee lakini nimeshafumba macho kuna faida gani sisikii sioni haya ya nini kwangu miye ! alisema Riyama

Riyama pia ametoa makavu live kwa baadhi ya wasanii wanaoleta maigizo misibani hasa wanapoona media hususani vituo vya TV hujipanga ili kuuza sura kwa sana tu "wakiziona kamera hujipanga kwa ajili ya kuhojiwa na waandishi basi hata kama marehemu alikuwa na ugomvi nae atajifanya jana kabla ya kufikwa na umauti walikuwa wote na kumwachia wosia kama rafiki"

Hata hivyo tabia ya kusifia wasanii wanapokufa pekee haipo kwa wasanii wenyewe kwa wenyewe hili limekuwa tatizo sugu hata kwenye media zetu na watu wa kawaida wakiwemo mashabiki msanii akiwa hai humponda muda mwingi na akishafariki huonesha kumpa sifa za kinafiki, tunatakiwa kubadilika kumpa mtu stahili ya sifa yake na kumkosoa penye kosa akiwa bado hai.
Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

1 comment:

  1. YEAH!, THAT TRUE, SHE'S SMART, GIVE HER ALL SHE DESERVE WHILE SHE STILL ALIVE.
    HERE IS ONE, U ARE SO BEAUTIFUL AND IMPRESSIVE.

    ReplyDelete