Pages

Thursday, June 5, 2014

Rais Kikwete Amkutanisha Diamond Platnumz Na Kevin Liles Meneja Wa Trey Songz, Big Sean Na Estelle.

Promoter DMK,Diamond Platnumz,Kevin Liles,Raisi Kikwete.

Kufutia Diamond Platnumz kuonyesha juhudi binafsi katika kuutangaza muziki wa Tanzania kimataifa Rais wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete nae ameaonekana kumuunga mkono tofauti na wale ambao siku zote wapo wakiishia kulalamika tu. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Diamond Platnumz ameweka picha akiwa na Rais Kikwete na Kevin Liles ambaye ni meneja wa Trey Songz, Big Sean na Estelle na pia mtu muhimu sana katika muziki industry ya marekani kwasababu aliwahi kuwa rais wa Def Jam Recordings kuanzia 1999-2004.
Kutokana na maneno aliyoandika Diamond ni wazi kuwa Rais Kikwete ndiye amemuunganisha na Kevin Liles baada ya kuona juhudi zake kimuziki ikiwemo kupendekezwa kwenye tuzo za BET Awards na MTV Awards 2014. "wapi utapata rais ambaye atakubali kutoa muda wake wa thamani ambao unatafutwa karibia na kila mtu duniani, akautumia kukusaidia kukutanisha na kuku-connect na mdau mkubwa duniani katika tasnia uliyomo ili kuhakikisha tu unafikia malengo na ndoto ya kazi Zako....Dah ahsante sana Mh.Rais, Mwenyezi Mungu akuzidishie na kukusimamia katika uongozi wako na siku zote za maisha yako" ameandika Diamond

Hii inaonyesha kuwa kuna kitu kikubwa kinakuja toka kwa Diamond na inaweza kuwa ni collabo na mmoja wa wasanii wanaosimamiwa na Kevin Liles au kitu kingine kikubwa zaidi. We are proud of you Diamond Platnumz.. 



                                        
                                                       



Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment