Pages

Wednesday, June 11, 2014

Mimi Ni Zao La George Tyson Kamwe Sitokuja Kumsahau: Lucy Komba

Lucy Komba
Actress maarufu Tanzania Lucy Komba amesema kuwa yeye ni zao la George Tyson na kamwe hatokuja kumsahau maishani kwasababu bila yeye asingejulikana. Lucy ambaye anatamba sokoni na filamu kibao akizungumza na Globalpublishers amesema kuwa alianza kuigiza kupitia mchezo wa Mambo hayo ambapo George Tyson alikuwa kama muongozaji hivyo kifo chake cha ghafla kimemuumiza sana
"Mimi ni zao la Tyson, nimeanzia katika mchezo wa maigizo wa Mambo hayo uliokuwa ukirushwa katika Kituo cha Runinga cha ITV na ndiyo ukawa mwanzo wangu kujulikana, asingekuwa yeye sijui ningekuwa wapi,
nitazidi kumuombea ili Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi" alisema Lucy

Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment