Pages

Tuesday, June 3, 2014

Akaunti Ya Facebook Ya Muigizaji Haji Adam "Baba Haji" Yavamiwa Na Matapeli "Hackers"

Haji Adam "Baba Haji"
Star wa filamu nchini Haji Adam "Baba Haji" amepatwa na masahibu baada ya akaunt yake ya Facebook kuwa hacked na matapeli ambao pia wanapost vitu vya kumchafua na kumdhalilisha. Kwa mujibu wa mtu wa karibu na Baba Haji akizungumza na swahiliworldplanet amesema kuwa matapeli hao walianza kwa kuandika post chafu za ushoga na kujifanya wao ni Baba Haji na sasa wameanza kupost kuhusu Zito Kabwe Foundation ili kuwatapeli watu ambao watadhani ni baba haji kweli ndiye amepost. Juhudi zinafanyika kuirudisha akaunti yake kama mwanzo.

Angalizo: Watu maarufu na hata watu wa kawaida wenye likes nyingi na marafiki wengi facebook ndiyo huwa wahanga wakubwa wa tatizo hili kwa kuwa siku zote hackers huwa-target watu wengi ili kufanikisha mambo yao kirahisi. Ukitumia link na mtu usiyemjua akikushawishi uifungue usiifungue kwasababu ukiifungua link hiyo inatafsiri moja kwa moja email na pasword yako na wao kuingia na kuichezea akaunt au page yako watakavyo. Wakati mwingine wanaweza kukutumia link na kukuambia tumeona picha zako chafu sehemu flani funguo hiyo link uangalie na wewe kwa mshangao wa kutaka kuona hizo picha chafu zinazodaiwa kuwa zako ukiifungua umekwisha kwasababu hutakuta picha zako chafu wala nini bali ni link ya ku-hack akaunt yako. Pia hakuna foundation za viongozi kama Zito ambaye mwenyewe alishasema mara kibao kuwa ni matapeli



Like our Facebook page Swahili World Planet for more updates about Tanzanian movie stars' latest gossips, news, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment