Pages

Wednesday, May 28, 2014

Ray Na JB Kutengeneza Filamu Mpya Nchini Turkey, Kupimana Ubavu Nani Zaidi.

Ray na JB wakiwa katika mavazi ya utamaduni wa watu wa Uturuki
Waigizaji wenye majina makubwa nchini Vicent Kigosi "Ray" na Jacob Stephen "JB" wanatarajia kutengeneza filamu mpya ambayo wataishuti nchini Uturuki(Turkey). Akizungumza na Bongo5 Ray amesema kuwa tayari filamu hiyo walianza kuishuti nchini Turkey sema walisitisha kidogo kufuatia kifo cha Adam Kuambiana ambaye alikuwa muigizaji na muongozaji wa filamu nchini hivyo JB Alilazimika kurudi nchini kama mwakilishi wao katika msiba huo lakini wanajipanga kurudi nchini humo muda si mrefu kumalizia filamu hiyo ambayo kwa mujibu wa Ray ni kupimana ubavu nani zaidi kati yake na JB.

"Mimi nilikuwa na movie na JB na tukaanza ku-shoot kule Uturuki lakini matokeo ya msiba wa Adam Kuambiana, tukasitisha zoezi na kuamua kutafuta tiketi kwa pamoja as a group za kuja kwenye msiba lakini kwa bahati mbaya tukapata tiketi moja tu ambayo tukajadili kwa pamoja tukaona atuwakilishe JB, sisi tuna utaratibu wa kufanya kazi, zamani nilikuwa na utaratibu na marehemu Steven Kanumba ya kufanya kila mwaka sinema moja na kupimana ubavu kwenye filamu moja, kwa hiyo baada ya kufariki Kanumba nikapanga na JB kila mwaka kutengeneza filamu moja ndiyo hiyo ambayo tumeianza na mambo ya misiba yakiisha tutarudi tena Uturuki kwenda kumalizia kazi. Hii ni mojawapo ya biashara na kuwatendea haki mashabiki wetu wa Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla kwa sababu tunapata comments nyingi sana kwenye Instagram, Facebook na twitter kwamba hebu jaribuni kucheza filamu moja Ray na JB tumuone nani zaidi. Nimecheza naye filamu nyingi lakini kwa kipindi hicho lakini kwa kipindi hiki kila mtu yupo juu. Ukiangalia JB ame-hit na mimi nipo juu pia kwahiyo tunahitaji kumtambua nani zaidi"

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Filamu ya SIO SAWA ipo sokoni nunua nakala yako halisi sasa


No comments:

Post a Comment