Pages

Tuesday, May 27, 2014

Modest Na Lufedha Kuanza Kushuti Filamu Itakayogharimu mil.60

Lufedha na Modest
Wasanii wakali wa filamu nchini Modest Bafite na Salehe Lufedha wanatarajiwa kuingia location tarehe 28 mwezi huu kushuti filamu mpya ambayo itawakutanisha mastaa nane wakali. Kwa mujibu wa chanzo filamu hiyo itagharimu shilingi mil.60 za kitanzania na itakuwa kali haijawahi kutokea kwa hiyo waandaji wake ambao husambaza filamu wenyewe ikiwemo ya Sio Sawa iliyoingia sokoni hivi karibuni na kufanya vizuri wanajipanga vilivyo kutoa kazi bora. Filamu hiyo itaongozwa na Modest Bafite ambaye amesomea mambo ya filamu nchini Denmark huku mwenyewe akiwa na asili ya Congo lakini akifanyia kazi Tanzania ambapo tayri alishafanya baadhi ya filamu na marehemu Steven Kanumba.

Filamu ya SIO SAWA tayari ipo madukani nunua nakala yako halisi ufaidi filamu hii kali.

No comments:

Post a Comment