Pages
▼
Sunday, May 25, 2014
Film Review: Kitendawili - Filamu Nzuri Ya Tanzania Usiyotakiwa Kuikosa Kuangalia.
FILM: Kitendawili
CAST: Single Mtambalike, Irene Veda, Haji Adam, Elangwa Mtahiko, Hisani Muya
DIRECTOR: Single Mtambalike
RATING: 4/5
Filamu ya Kitendawili ambayo imetoka hivi karibuni ni moja ya filamu nzuri kabisa kutoka mwaka huu. Katika filamu hii Single Mtambalike "Richie" amekuja na kazi nzuri tofauti kabisa na alivyozoeleka kucheza filamu na characters za kwenye makochi kama baadhi ya wasanii wenzake wengi wenye majina wanavyofanya mpaka sasa. Story ya filamu inamhusu Richie akiwa amecheza upareni kilimanjaro, anampenda msichana ambaye ni mkimbizi(Irene Veda) aliyeko kigoma na kuja nae kwao upareni na kuoana. Hata hivyo maisha yanakuwa magumu kijijini hivyo Richie anaamua kwenda mjini kutafuta maisha na huku nyuma kumuacha mkewe akiwa na mama na baba yake Richie, baba mtu ni mlevi sana kiasi cha kushindwa kuihudumia familia na hampendi mke wa Richie. Richie anakaa mjini na kufanya kazi sehemu flani lakini siku moja anaona pesa za sehemu anayofanyia kazi na kuzichukua baadaye anafungwa miaka miwili jela, anatoka na kuamua kurudi kijijini ambako anamkuta mkewe(Irene Veda) ni mjamzito na anaishi na mwanaume mwingine(Haji Adam) baada ya kusubiri kwa muda mrefu na kukosa mawasiliano na Richie ambapo mama yake pia tayari alishafariki dunia pamoja na mtoto wa Richie kwa kukosa huduma bora. Visa vinavyotokea kati ya Irene, Richie na Haji Adam"Baba Haji" ndiyo vinaifanya zaidi filamu hii ikufanye ukubali kuwa filamu zetu zitafikia hatua ya kuitwa filamu. kisa ni cha kusisimua sana.
What is good: Story ya filamu na mwandishi wa script alijitahidi sana kuifanya script kuwa tight, mtu wa picha alifanya kazi nzuri ingawa kuna sehemu chache sana kwa mbali picha hazikuonekana vizuri sababu ya mwanga ila si rahisi kulijua hili, locations asilia na za kuvutia, editor alifanya kazi nzuri, director alistahili nomination ya tuzo. Na kingine kabisa ni filamu hii kutokuwa na part 1&2 hongera sana Proin Promotions(msambazaji) kwasababu wasambazaji wengi nchini hushinikiza kuweka part
1&2 na mwisho kuharibu filamu.
Performances: Katika hii filamu Richie amecheza vizuri yaani moja ya performances nzuri sana kwa waigizaji wa kiume mwaka huu na kwake mwenyewe Richie . Hata hivyo ni Irene Veda aliyecheza kama mke wa Richie ambaye alikuwa kivutio zaidi kwa kuubeba uhusika wake vizuri na uhalisia kama mwanamke aliye njia panda kwa wanaume wawili kwa wakati mmoja huku akiwa mjamzito na misukosuko ya mapenzi. in short Irene stole the show !. sina uhakika ila nafikiri Irene ni muigizaji mpya lakini kwa performance yake basi hata angeshinda tuzo ya best debut na best actress of the year ni stahili yake, I'm sure kina Irene Uwoya, Wolper, Wema Sepetu na waigizaji wengine wenye majina wakimuona Irene Veda katika hii filamu licha ya kwamba hana jina kama wao lakini watakuwa na cha kujifunza kutoka kwake. Irene Veda ni mrembo na mwenye kipaji asilia hivyo kipaji hiki kisipotee media zimpe support na wadau wa filamu wampe nafasi zaidi atuelimishe na kutuburudisha pia. Kwa upande wa Haji Adama alicheza vizuri pia, na wasanii wengine akiwemo kupa.
Last word of the film: Kama hujaiona hii filamu basi kainunue sasa utacheka, utasikitika, utaburudika na mwisho kupata fundisho, hata kwa wale ambao siku zote huishia kuponda filamu za kitanzania basi hapa kwa namna moja au nyingine kuna sifa watatoa licha ya kuwa makosa hutokea popote hata Hollywood yapo. Waandaaji wa hii filamu wanatakiwa pia kujaribu kuipeleka kwenye tuzo na film festival kadhaa kwani inaweza kushinda baadhi ya vipengele.
No comments:
Post a Comment