Wema na Martin Kadinda |
"Good morning all of ypu....I just woke up like "Hasiralees" kwakuwa hili vuguvugu la kutokuwa na maelewano mazuri kati ya Wema Sepetu(my client) na Kajala limekuzwa katika social networks basi na mimi naomba nitoe taarifa kutoka kwetu Endless Fame.
Katika urafiki kuna mengi yanajitokeza na endapo kutakuwa na hitilafu sehemu basi ni muhimu kupeana nafasi ili kila mtu aweze kujirekebisha na mwisho wa siku maisha yaendelee hilo ndiyo lililotokea baina ya hawa wawili. Lakini Katika kipindi hicho cha so-called mapumziko kuna mambo mengi yamejitokeza, yapo ya kweli na yapo yaliyotengenezwa na baadhi ya watu, kuna media coverage juu ya hawa wawili na Wema sikumpa nafasi ya kuzungumza na chombo chochote cha habari kwakuwa nilijua litakuzwa zaidi, ila tulipoona shutuma zinazidi kuja upande wake akafanya interview na gazeti moja na kuelezea upande wake na mwisho alisema hana tatizo na Kajala sema tu kwasasa anahitaji space.....tukawa tumefunga mjadala huo
Tunaumizwa na blogs na magazeti yanapoandika stori kama vile wana ushahidi kutoka Endless Fame au mtu wa karibu na Wema. Team Wema wote waliopo Instagram sijawahi kuonana na hata mmoja kati yao hivyo hakuna anayewatuma wala kuwashinikiza ila wao wanafanya kile kinachowapendeza au hatuwezi kuwakataza kwasababu ni maisha yao binafsi na ni mapenzi yao ya dhati kwa Wema.
Poleni kwa wote mnaoumizwa na haya yanayoendelea ila nadhani tukazane na kazi zetu na maisha yetu maana haya ya Instagram tuyaache huku huku ukiyapatiliza utashindwa kumwamini hata mama yako mzazi"
Hivi karibuni Kajala kupitia kipindi cha TakeOne cha Clouds Tv alisema kuwa ugomvi wao Wema umekuzwa na watu na media na sio kama inavyodaiwa kuwa amemchukulia Wema mwanaume. Kajala alisema kuwa walitofautiana kwa mambo madogo tu ya kawaida lakini wamejikuta wakiwa na ugomvi kweli kutokana na media na watu kuukuza ugomvi huo, Kajala alisema kuwa anaumizwa sana na hali hiyo.
Wema na Kajala |
No comments:
Post a Comment