TRA sasa hivi wanakiri udhaifu wa kutokamata bidhaa feki wakidai
bado wanajipanga kitendo ambacho kiliamsha hasira za wadau wa
filamu kiasi cha kumfanya Afisa wake, bwana Mdee aingie mitini
kabla ya kikao kuisha.
Moja ya sababu iliyowafanya wadau kumshambulia mtumishi wa
mamlaka ya Mapato TRA ni kauli aliyoitoa wakati akiwalisha mada
kuhusu maharamia pale aliposema kuwa suala la kugushi stepu
mtuhumiwa wa kwanza ni mmiliki wa filamu hiyo au aliyeomba na
kupewa ridhaa ya kuisambaza.
Mmoja kati ya watu waaliompingaa ni pamoja na mwanadada Leoni
ambaye ni msambazaji kutoka kampuni ya Leo Media ambaye alishindwa
kuelewa msaada wa mamlaka hiyo na kuamsha hisia za watu wengine
waliotaka kujua faida za TRA kwa watengenezaji wa filamu. akijibu swali
hilo alisema
“Sisi kama chombo ambacho kipo kwa mujibu wa sheria tunafanya
mambo kwa mipangilio na si kukurupuka tu, tunahitaji kuweka
ambao hauna hasara lakini pia tunahitaji utafiti makini kabla
ya kuingia kukamata watu,”alisema Mdee.
Moja ya changamoto iliyokuwa tatizo ni suala la mamlaka kushindwa
kukamata Dvd feki ambazo zipo kiholela katika maduka mbalimbali nchini ikiwemo
kariakoo, huku wasanii wakisubiri wa ndani wakipanga foleni kwa
mdosi bila mafanikio kwa mantiki hiyo mamlaka isipofanya hivyo ni
hatari kwa maendeleo ya tasnia ya filamu.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Taifa
source: Filamucentral
No comments:
Post a Comment