Saturday, March 15, 2014

Rais Wa Shirikisho La Filamu Tanzania Alaani Waandishi Wa Habari Za Filamu Wasiofanya Tafiti Katika Uandishi Wao.

Simon Mwakifwamba ambaye ni rais wa Shirikisho La Filamu Tanzania(TAFF) na pia muigizaji na na muongozaji wa filamu nchini
HASSAN BUMBULI NA UANDISHI USIO NA TAFITI:

Nianze kwa kusema nimesikitishwa sana na makala ya mwandishi wa habari za sanaa aliyepata elimu ya miaka mitatu tasisi ya sanaa bagamoyo kwenye gazeti la leo la Mtanzania kwamba wasanii tumekumbuka shuka wakati kumekucha na kwamba alitushauri si kweli. Ndio maana ninasema kwa ujasiri na uhakika hakuna tafiti na ukweli kwenye makala yake,mashirikisho manne tuliunda baraza la katiba pale BASATA tulipokea maoni ya wadau wa sanaa zote na kuweka vipaumbele vyetu kwenye rasimu ya katiba na tukawasilisha rasmi kwenye ofisi za tume ya Warioba na kugongewa nakala yetu moja muhuri wa received yenye kuonyesha tarehe ya kuwasilisha, Bumbuli hizi habari anazoandika kazitoa wapi? Ninaanza kuwa na mashaka huenda si mwenzetu,wala uchungu wa sanaa ya Tanzania haujui japo ni mwandishi wa habari za sanaa.

Hatua ya pili tulipeleka barua ya kuomba uwakilishi kwenye bunge la katiba kwa katibu mkuu kiongozi ikulu kwa kila shirikisho kupeleka majina tisa. Jumla ya majina 36 kwa mashirikisho yote manne na kupata nafasi moja tu, bumbuli anayatoa wapi maneno ya kusema ubinafsi kila msanii alienda kivyake, masharti ya kuomba ili kuwa ni taasisi na si mtu binafsi unaweza kuona lack of information, sisi tunajua tunachodai pia sisi si wanyasa au wakongo ni watanzania wa kuzaliwa na si wa kuomba uraia ,tuna haki ya kudai katiba itutambue wasanii na kulinda miliki bunifu, wabunge wa Bunge la katiba wametusikiliza na kutuelewa kwa kuwapa facts na research mbalimbali pamoja na copy iliyogongwa muhuri wa tume ya katiba. Kutusahau kwa tume ya Warioba sio kwamba hatuna nafasi tunayo, hivi ikatokea leo hoja zetu zikapita Bumbuli utawaambia nini wasanii wa Tanzania? Makala yako haitujengi inatubomoa na kutukatisha tamaa pia kutufanya sisi wasanii hatujui tunachodai ila wewe unajua zaidi.

Leo unashangaa kutunga nyimbo na filamu ulitaka kampeni yetu ifanywe na nani? Na wewe Hassan bumbuli? kitendo ulichofanya si cha kiungwana wala uzalendo kumbuka kuwepo kwa wasanii kumekupa fulsa ya wewe kupata ajira ya mwandishi wa habari za sanaa na wasanii.
Tunataka utuombe radhi kwa kuandika makala isiyo na tafiti, ushahidi na vielelezo ninavyo kwa haya niyasemayo, toa ushahidi wako kwa haya uliyoandika.

TUNA LAANI KWA MAKALA YAKO YA GAZETI  LA MTANZANIA LA TAREHE 15/3/2014 SIKU YA JUMAMOSI, UMEICHAFUA TASNIA YA SANAA NA WASANII WOTE NCHINI.

Simon Mwakifwamba
Rais TAFF



 

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment