Pages

Monday, March 24, 2014

Mainda Achoshwa Na Waandishi Wa Magazeti Ya Udaku Wanaomuandika Habari Za Uongo

Mainda
Star wa filamu nchini Mainda anaonekana kuchoshwa na habari za uongo katika magazeti ya udaku na kuamua kuwapa live wahusika! leo gazeti moja lilitoka na habari kuwa ni mjamzito huku jingine likitoka na habri inayomhusisha na Ray. Kupitia Instagram star huyo wa muda mrefu aliandika......
"@shakoor Jongo nakueshimu sana tena sana ila kwa kuwa umeandika habari kwa faida yako mwenyewe Mungu akubariki ila nasema hivi hakuna mtu atakayeweza kunichafua katika huu ulimwengu. Umeandika habari yenye uongo mwanzo mwisho kwa mfano nikienda kukufungulia mashitaka utaniona mbaya halafu mnazitaja hosptali za watu hamuoni kama mnazichafulia majina sasa nikienda hapo kwa Mvungi wewe ndio uliyenipeleka na hiyo mimba itakuwa wewe ndio ulionipa.... acheni utoto halafu kitu kingine sijaongea na gazeti lolote sasa unaposema umeongea na mimi wapi kwa nini mnapenda kubuni mambo. plz plz sipendi mnapoandika upuuzi mkanichanganya na majina ambayo sihusiani nayo. Kila mtu anamaisha yake hivyo sipendi kuchanganywa kwenye upumbavu halafu unasema ulikuja kwangu ukaambiwa sipo labda nilikuwa kwako kama nilikuwa sipo. Tusipende kukwazana katika maisha. Kiukweli kwa hili umenikwaza sana.
 
 Mungu wangu anaujua ukweli hata unichafue kwa njia zozote sichafuki, taarifa tu ya haraka haraka mi siyo mzinzi kwa sasa huko nilishapita kitambo eeeeeeeh halafu mimba ni jambo la kheri siyo Ukimwi huo useme niufiche. Nitazaa ndani ya ndoa na si nje ya ndoa maana hata mimi nimezaliwa ndani ya ndoa why me nizae Nje ya ndoa ha ha ha ha haaa ! me siyo kuku wala mnyama nijizalie ovyooooo. Halafu umeandika nimetoa mimba labda wewe ndio Ulikuwa Dk wangu ulinifanyia hilo tukio.....Mungu akubariki kwa habari yako ila hili gazeti watu watalisoma Leo kesho wamesahau na maisha yataendelea. Maana wiki iliyopita mliniandika nikakaa kimya sasa naona story mnaifanya endelevu kama tamthilia ya Isidingo vile."
 
Uwiiiii Leo naona mmeamka na mimi nyinyi magazeti hivi naomba kuuliza bado tu mkiandika habari za Ray na mimi mnaniweka kiruuuuuu mbona mimi nimeshasahau hata kama nilisha kuwa na mahusihano na huyo mtu......jamani hebu acheni maisha ya endeleeeeeeee me huko sipo tena halafu huwa sipendi mkiandika habari zake nikawekwa sura yangu au jina langu coz me sihusiki katika mambo yake na mimi siyo mzazi wa hao watu useme wakiandikwa kwenye magazeti me ni Ubini wao kwamba majina yao yakiandikwa langu lisipokuwepo jina halijakamilika mbona hamtaki kuukubali ukweli !
 
Ni hivi fungeni ukurasa wa habari za huyo kaka na wanawake zake me kuniweka sihusiki na nilishalizungumzia hilo toka mwaka jana lakini naona mkitaka kunogesha habari zenu za uongo mpaka muweke jina langu...ha ha ha ha ha ha ha ha mnajua mnanichekesha sana. msinitafutie uadui na watu wapendwa coz me sitaki kujenga uadui na watu basi msinilazimieshe. Natamka tena mimi na Ray we are over toka mwaka jana so acheni hayo mambo ya kuniandika nae. Andikene mambo yake na maisha yake na watu wake siyo uungwana kuniandika kunichanganya na mimi.@Gazeti la Kiu.
 
 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more
 

1 comment:

  1. Out of topic nahitaji kujua Mwenyekiti wa bongo movie Steve Nyerere imekuwaje ampatishe Uwoya na Wolper wakati yeye mwenyewe ana bifu na Batuli: Unafiki wake wa kupatanisha watu huku yeye mwenyewe hana maelewano vizuri na Batuli Davina na Sandra binafsi nahisi kundi la bongo movie ni la watu washenzi na wasioona utu wa wenzao tuwekee majibu tafadhali

    ReplyDelete