Pages

Thursday, March 27, 2014

Jackline Wolper Na Irene Uwoya Wazika Tofauti Zao Za Muda Mrefu Baada Ya kupatanishwa.

Irene Uwoya na Jackline Wolper
Ule uhasimu uliokuwepo kwa takribani miaka miwili sasa kati ya mastaa wakubwa na warembo Swahiliwood Jackline Wolper na Irene Uwoya hatimaye umefikia tamati baada ya kupatanishwa juzi. Wawili hao walidaiwa kuingia katika beef zito baada ya Uwoya kumsema Wolper vibaya kwenye media ambapo pia aliwahi kukaririwa na gazeti moja akiwa jijini Arusha akisema kuwa Wolper amemroga ili amshushe kwenye sanaa na yeye(Wolper) kuwa juu kisanaa kitu ambacho kilidaiwa kumuudhi sana Wolper.


 Chanzo kimoja kilicho karibu na mastaa hao kikizungumza na Swahiliworldplanet kilisema kuwa aliyewapatanisha ni Steve Nyerere na wote wawili wakakubali kuondoa tofauti zao. "Wolper na Irene Uwoya wameitwa na kupatanishwa na Steve Nyerere sasa wako poa, unajua Wolper alikasirishwa na kitendo cha Uwoya kwenda kwenye media na kumchafua kwa mambo ambayo hakufanya kipindi cha nyuma" kilisema chanzo hicho huku kikikataa kuwekwa jina lake kweupe.

Tungependa kuwapongeza mastaa hawa kwa uamuzi wao mzuri wa kuzika tofauti zao na kuendelea kukuza sanaa ya filamu Tanzania


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

1 comment: