Pages

Tuesday, March 25, 2014

Acheni Kuokotaokota Sio Kila Msichana Mzuri Ana Kipaji Cha Kuigiza: Simon Mwakifwamba

Simon Mwakifwamba
Muigizaji na muongozaji wa filamu nchini ambaye pia ni Rais wa shirikisho la filamu Tanzania(TAFF) Simon Mwakifwamba amekemea baadhi ya watengenezaji wa filamu nchini wanawachukuwa wasichana wazuri barabarani na kuwapa nafasi ya kuigiza kwenye filamu bila kuwa na vipaji na matokeo yake ndiyo huchafua sanaa kwa skendo za mara kwa mara. Akizungumza na Globalpublishers Mwakifwamba alisema "Nakemea  wasanii kufanya mambo yasiyofaa mbele ya jamii. Lakini lipo tatizo moja... unajua mimi nipo kwenye sanaa mwaka wa 28 sasa, nina uzoefu wa kutosha.
“Siku hizi mambo yamebadilika. Zamani wasanii tulikuwa tunalelewa kwenye makundi, tulikuwa na wazee wetu ambao walisimamia nidhamu


“Sasa hao ambao wanaokotwa huko barabarani kwa sababu ya uzuri ndiyo wanaokuja kuharibu sanaa. Watayarishaji wabadilike. Siyo kila miss ni msanii. Siyo kila msichana mzuri anaweza kuigiza. Wazingatie weledi, siyo mwonekano."




Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment