Batuli |
Chanzo hicho kiliendelea kwa kusema kuwa kilikutana na waheshimiwa hao wawili kwa nyakati tofauti katika hoteli moja iliyopo Dodoma na kumuomba awasaidie namba ya Batuli kwa madai urembo wake unawanyima usingizi "me nipo Dom kwa issue zangu binafsi nimekutana na waheshimiwa wawili(hakuwataja majina) wame-data na uzuri wa Batuli wakataka niwape namba yake nikawaambia sina, mie sipo karibu na Batuli"
Baada ya kuzipata habari hizo Swahiliworldplanet ilimtafuta Batuli na kumueleza kuhusu habari za uzuri na urembo wake kuwachanganya baadhi ya waheshimiwa huko Dodoma, star huyo wa filamu za Bad Luck na 5 Days Family alijibu huku akionyesha kushangazwa na habari hizo kwa kusema "sikwenda Dodoma kufanya uhuni kama baadhi ya mastaa wenzangu wafanyavyo wanapokuwa Dodoma, sina uhakika kuwa namba yangu ya simu ilikuwa inatafutwa na wabunge/mawaziri kwasababu kila kiongozi tuliyekutana nae hakutoka nje ya topic kabisa vile vile sikuwa peke yangu tulikuwa wengi zaidi ya 12 na kila kikao tulikaa wote kwa pamoja"
Batuli ambaye ni mmoja wa mastaa wa filamu nchini waliojipatia umaarufu kwa kazi zao na sio skendo kama baadhi ya mastaa wenzake alimalizia kwa kusema "watu huzusha maneno kutokana na mitazamo yao ila ni vyema mtu kuongea lenye ukweli, binafsi sijaona kiongozi aliyekuwa na muda wa kupoteza kwa ufupi waheshimiwa wote wapo busy sana, sisi wenyewe tulikuwa hoi kwa vikao kuna wakati tulikuwa tunamaliza vikao saa 6 usiku, kwa ufupi naweza kusema aliyefikisha taarifa hakufanya research kutosha, vile vile tuliochaguliwa kwenda Dodoma hasa hasa kwa upande wa wasichana ni mimi na Monalisa hivyo unaweza kupata picha halisi ya tuliochaguliwa na muonekano wetu mbele ya jamii"
Batuli
Batuli mzuri sanaaa kina Wema na Uwoya watasubiri sana
ReplyDeleteKiukweli ni kifaa cha kuuliwaza mwili na moyo.
ReplyDelete