Pages

Thursday, February 6, 2014

SIASA ZIMENIPOTEZA KISANII: MARLAW

Marlaw
Wakati wasanii mbalimbali wa filamu na muziki nchini wakijiunga na vyama vya siasa, mwanamuziki Marlaw amefunguka kwa kusema kuwa siasa ndiyo imempoteza katika ramani ya muziki. Akizungumza na Mwanaspoti amekiri kuwa kitendo chake cha kujihusisha na masuala ya kisiasa mwaka 2010 ndiyo chanzo cha kushindwa kufurukuta kimuziki.



"Nilikuwa juu sana nilifanikiwa kuuza nakala nyingi sana za albamu yangu ya kwanza "Bembeleza", lakini naamini kitu kilichonishusha kwenye ramani ya muziki ni siasa" alisema

"kwa maono yangu naona pale ndiyo nilikosea kwani mashabiki wa muziki ni wanachama wa pande zote na wengi si waelewa, msanii kushiriki siasa ni haki yake kwani anatafuta pesa lakini mpinzani anakuchukia. Unajua hakuna kitu kibaya kama masuala ya kidini, kikabila, kisiasa hata ukereketwa kwenye masuala ya mpira unaweza kugombana na mtu kwasababu ya haya mambo" aliongeza

"Mambo ya siasa bwana acha kabisa, lakini mimi ni msanii ninaweza kuburudisha watu wa aina yoyote hata kama ni wa chama kingine, kikubwa watu wanatakiwa kutambua kwamba msanii anatafuta pesa hata akiitwa kwenye sehemu nyingine yenye upinzani mkubwa kwa kiasi gani, atakwenda kwakuwa anatafuta pesa na kesho huenda ukamkuta upande mwingine haimaanishi kwamba amehama"

"Kikubwa ni ikiwa msanii amechukua kadi kutoka chama husika na kujitangaza kwamba yeye ni mkereketwa wa chama hicho, hata hivyo kwa upande wangu naoni ni haki ya msanii kujiamulia kwamba anataka awe mfuasi wa chama gani, haigombi na wala haina masharti eti ili uwe msanii lazima ujiondoe kushiriki siasa, sio kweli"

"sifikirii kabisa kama ninaweza kushiriki tena kwenye uchaguzi, kilichopo sasa ninajiuza mimi na kazi yangu. Hivi sasa nimeshaandaa albamu yangu mwenyewe yenye nyimbo nyingi tu" alisisitiza

Marlaw aliwahi kutamba na nyimbo nyingi zikiwemo Bembeleza, Rita, Missing My Baby(Pii Pii), Sorry Sana, Kirungu, Nifundishe na Busu La Pink.

Marlaw katika kampeni za CCM kwenye uchaguzi mkuu 2010


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

1 comment:

  1. Acha kisingizio kijana.
    Kwa kinywa chako ulitangaza unastaafu game
    Mnawachanganya mashabiki wakihama inakuwa siasa..mbina diamond mlikuwa naye na bado ana hit...nidham kazin ndo wot count

    ReplyDelete