Pages

Sunday, February 9, 2014

NILIROGWA KATIKA LILE SAKATA LA KUJIUZA KWA MIL.10: BABY MADAHA

Baby Madaha
Baada ya hivi juzi kati gazeti moja kuripoti kuwa actress/singer Baby Madaha alinaswa katika issue la kujiuza kwa dau la shilingi milioni 10. Sasa Baby Madaha amesema ni kweli uchawi upo kwani anahisi kupigwa kipapai katika lile issue lake la kujiuza kwa madai alikuwa hajielewi elewi wakati alipokutwa na dhahama hiyo. Akizungumza na mtandao wa Bongomovies Madaha alisema kuwa jamaa aliyetajwa kujiuza kwake aliwasiliana nae kwa ajili ya kutaka kusambaza filamu yake mpya ya Gal Bladder na kukutana nae lakini alishangaa baadaye habari kutoka gazetini anajiuza "Yaani hata sielewi ilikuaje nikaenda kukutana na yule jamaa, ilikuwa ni kama muujiza hivi, mwanzo nilisita sana ila nikashangaa nimefika tu pale bila kujielewa, ni vitu vya ajabu sana"



Madaha anayesifika kwa kupenda kukwaruzana na wasanii wenzake aliongeza kwa kusema...
"Hata wafanyaje, waniroge, wanichafue, i'm a bad gal, na sibabaishwi na vijimaneno vya watu hata kidogo, sitoki candy n Candy hata waroge kwa waganga wote duniani. Kama walifikiri nimeumbuka, wajue watasubiri sana. Nikitoka kenya naenda Holywood tu!"

Msanii huyo alimalizia kwa kusema kuwa matatizo yote yaliyotokea na record label yake ya Candy n Candy baada ya issue ya kudaiwa kujiuza wameyamaliza na sasa mambo yapo shwari na wapo pamoja kama kawaida na Joe Kariuki ambaye ndiye mmiliki wa Candy n Candy ya nchini Kenya huku wakidaiwa kuwa wapenzi na Madaha.

No comments:

Post a Comment