Pages

Wednesday, February 12, 2014

MTUNISY APANGUA MADAI YA KUACHANA NA MKE WAKE.

Star wa filamu nchini Nice Mohamed 'Mtunisy' anadaiwa kuachana na mke wake hivi karibuni. Chanzo kimoja kiliuambia mtandao huu kuwa Mtunisy siku hizi yupo mwenyewe wameshaachana na mkewe sababu zikidaiwa ni scenes za kimapenzi anazocheza Mtunisy na waigizaji wa kike ikiwemo filamu ya Who's Bad kwa madai kuna scenes katika filamu hiyo mkewe hakuzifurahia na kumnyima usingizi. "Mtunisy yupo single wameachana na mkewe hivi karibuni, unajua Mtunisy kuigiza scenes za kimapenzi na wasichana wazuri kumekuwa kukimnyima raha mkewe, kuna filamu ya Who's Bad ndiyo imefanya mke wake uvumilivu kumshinda" kilisema chanzo hicho juzi.

Mtunisy alipotafutwa na kuulizwa kama ni kweli ameachana na mke wake alikana madai hayo na kusema mtoa habari hizo atakuwa mwehu "Sio kweli huyo aliyesema hivyo atakuwa mwehu kidogo" alisema Mtunisy anayetamba katika tasnia ya filamu nchini ambapo baadhi ya watu humfananisha na Ramsey Nouah wa Nollywood kimuonekano na hata kiugizaji hasa katika scenes za kimapenzi.

                                                        Mtunisy
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

3 comments:

  1. Ni kweli wameachana na amerudiana na mwanamke wa maisha yake Yobnesh Yussuph au maarufu kama Batuli katika maisha ya Mohamed Yussuph au maarufu kama Mtunisy mwanamke wa maisha yake alikuwa ni Batuli na waliwahi kukaa kwenye mahusiano kwa miaka 4 kama Mke na Mume na walipata mtoto ingawa alikuwa bahati mbaya hakuna msanii asiyejua haya hasa hasa tuliokuwa nao Maple Sanaa Group

    ReplyDelete
  2. asante mjumbe kwakutupa habari hii na kutuhakikishia

    ReplyDelete
  3. UMENIKUMBUSHA MBALI ULIYETAJA KAOLE SANAA GROUP ILA MAPENZI YA MTUNIS NA BATULI HAYAKUWA SIRI NAKUMBUKA WALIPAMBANA BATULI NA PAULINE ZONGO NA BAADHI YA MAGAZETI YALIANDIKA NIMEAMINI TRUE LOVE NEVER DIE WAOANE SASA

    ReplyDelete