Pages

Monday, February 17, 2014

LULU ATINGA MAHAKAMANI, KESI YAKE YAAHIRISHWA.

Lulu, Dr.Cheni na mama mzazi wa Lulu wakipitia gazeti wakati wakisubiri kuanza kwa kesi

Lulu akiwa na mama yake mzazi

Lulu akiwa na Dr.Cheni
Dr.Cheni na mama yake Lulu



Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabiri muigizaji wa kike, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu imesikilizwa leo (February 17) katika mahakama kuu, Kanda ya Dar es Salaam.
 
Lulu alikiri mbele ya Jaji Rose Temba kuwa alikuwa na uhusiano wa mapenzi na marehemu Steven Kanumba na kwamba walikuwa na ugomvi, lakini alikana mashitaka ya kumuua bila kukusudia.
 
Mbali na kukiri kuwa na uhusianano wa mapenzi, muigizaji huyo pia alikiri kuwa baada ya tukio hilo alitoka nje ya chumba walichokuwepo na kwenda kumwambia mdogo wake marehemu Kanumba, Setti Bosco kuwa Kanumba ametangulia mbele ya haki.
 
Akisoma hati ya mashitaka, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Monica Mbogo, alidai kuwa Aprili 7, mwaka 2012, Sinza Vatikani, Mkoa wa Dar es salaam, mshitakiwa alimuua bila kukusudia Stevin Kanumba.
 
Wakili Kombo, alidai kuwa pamoja na mambo mengine, marehemu Kanumba baada ya kufa, mwili wake ilipelekwa hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo majibu yanaonyesha kwamba kifo chake kimesababishwa na uvimbe ndani ya ubongo.
 
Upande wa serikali una mashahidi watano pamoja na vielelezo wakati upande wa utetezi pia unatarajia kuwa na mashahidi watano na vielelezo.
 
credit: Jestinageorge blog 
 
 
 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment