Inadaiwa wasanii hao wameanza kuonekana ni muhimu katika kipindi hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2015 ambapo kundi la wasanii huwa na ushawishi katika jamii hivyo chama hicho kuwatumia ili kupata kura zaidi.
Ukiachilia mbali waliolalamikia wasanii hao kuwa hawajitambui kwa maana kuwa watatumiwa katika kipindi hiki cha shamra shamra za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 na baada ya hapo kuonekana hawana thamani tena lakini wengine wameona ni sawa tu walivyoamua kwani ni haki yao kikatiba kuchagua chama chochote kile. Inadaiwa kuwa wasanii wengi waliojiunga CHADEMA ambacho ndiyo chama pinzani kwa CCM ni wanaharakati tangu hawakujiunga na wana uchu wa kumkomboa msanii ili afaidike na kazi zake, wasanii waliojiunga CHADEMA ni kama vile Lady Jaydee, Afande Sele, Professor J, Sugu ambaye kwasasa ni mbunge wa mbeya mjini na wengineo.
Naye Joyce Kiria ambaye anadaiwa kuwa mwanzilishi wa jina Bongo movies amewachana wasanii hao kwa kuandika ...............
Kila mtu anao uhuru wa kuchagua chama atakacho hasa akiona kama kinamfaa, Je wewe una maoni gani kwa wasanii hawa ambao kila siku wanalia kazi zao kuibiwa, kutonufaika na kazi zao lakini serikali iliyopo madarakani haiwasikilizi?, Unadhani kujiunga kwao CCM itakuwa suluhisho la matatizo yao?
No comments:
Post a Comment