Sunday, February 9, 2014

JAMANI MIMI SIO JINI KWELI BALI NINAIGIZA FILAMU TU: SHASTA

Shasta
Muigizaji maarufu wa filamu nchini, Shasta amefunguka kuwa baadhi ya watu na mashabiki wake wanadhani kuwa yeye ni jini kweli baada ya kuigiza filamu kadhaa kama jini na kuuvaai uhusika vizuri. Akizungumza na Swahiliworldplanet Shasta alisima kuwa anakwepa hata baadhi ya maswali ya watu ambao wanadhani yeye ni jini kweli "Nakwepa maswali ya watu maana wengi wanaamini mimi ni jini kweli". Shasta alimalizia kwa kusema "Nawaambia mimi sio jini ni binadamu wa kawaida tena ni Msukuma wa Bariadi"


Shasta ambaye pia hutumia jina la Karina Hundaya amecheza filamu nyingi kama jini, filamu hizo ni kama vile Kisasi Cha Mzimu ,Siri Ya Majini, Pete Ya Ajabu ,Sekunde Chache.

                                                                Shasta

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment