Pages

Friday, February 14, 2014

FILAMU YA NJIA PANDA KUINGIA SOKONI KESHO, WASTARA, OMARY CLAYTON, HEMEDY NA FRANK WAKUTANA HUMO.

Muigizaji, mtunzi na director maarufu nchini Omary Clayton amekuja na filamu mpya nyingine inayotarajiwa kuingia sokoni kesho tarehe 15 February. Filamu hiyo inaitwa Njia Panda na ukiachilia mbali Omary mwenyewe mastaa wengine katika filamu hiyo ni Wastara Juma, Hemedy Suleiman na Mohamed Mwikongi(Frank). Filamu hiyo imeandikwa na kuongozwa na Omary Clayton.

 Akizungumza na mtandao huu Omary ambaye alianza kutamba na kundi la Kaole kabla ya kujitosa kwenye filamu jumla jumla alisema "Nimeigiza tofauti sana humo Kama zezeta, and nimeandika, nime-direct pia, ni cinema yenye maisha magumu sana na mateso, huku haki yangu mwenyewe ndio inanitoa machozi na manyanyaso kila muda, and inatoka kesho rasmi"

Mzigo ndiyo huo unaingia sokoni kesho so wewe mdau wa filamu na Tanzania hakikisha unapata copy yako original. 0656 312251



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

No comments:

Post a Comment