.
Akizungumza na mtandao wa filamucentral kwa masharti ya kutotajwa jina lake, msanii mmoja ambaye pia alishiriki katika kuigiza filamu hiyo alifunguka kuwa chanzo cha kusambaratika kwa kampuni hiyo ni kitendo cha Tico ambaye alikuwa mpigapicha na mhariri wa filamu hiyo kuandika kuwa filamu hiyo imeongozwa na Issa Musa au Cloud 112 ambaye ni prodyuza wa muvi hiyo badala ya Jackson Kabirigi ambaye ndiye aliongoza filamu hiyo.
Inasemekana kuwa baada ya kuona kosa hilo Jackson Kabirigi ambaye anang’ara na filamu ya Kisate alimkabili Tico kumuuliza kulikoni lakini badala ya Tico kufanya marekebisho alisema kuwa yeye anafuata alichoambiwa na Cloud 112 jambo ambalo ni kinyume na kanuni za filamu duniani kote kwa mtu kumpa sifa asiyestahili.
Baada ya majibizano makali kati ya wamiliki hao inasemekana kuwa kila mmoja aliamua kushika yake wakiiacha kampuni iko hewani.
Mtoa taarifa wetu aliyejibainisha kuwa anamkubali sana Kabirigi alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa huo ulikuwa ni mpango ambao tayari ulishawekwa toka awali katika kumhujumu Kabirigi baada ya kuonekana kung’ara katika upande wa uongozaji wa filamu hasa baada ya filamu aliyoiongoza ya Mdundiko kushinda tuzo kadhaa za kimataifa.
FC ilijitahidi kuwapata Jackson Kabirigi na Timoth Conrad bila mafanikio ila ilifanikiwa kuwasiliana na wasanii Wastara na Hidaya Njaidi ili kujua ukweli kuwa ni nani aliyeongoza filamu hiyo kati ya Jackson Kabirigi aliyeandikwa kama ‘2nd Director’ na Issa Mussa Cloud 112 aliyeandikwa kama ‘Director’ ambapo walifunguka kama ifuatavyo,
Wastara alisema ‘’Sinema iliongozwa na Jackson Kabirigi sijui wenyewe walivyoamua, ‘’
Pia aliulizwa mwigizaji mwingine ambaye ni Hidaya Njaidi naye alifunguka hivi
“Director ninayemjua ni Jack ambaye aliongoza filamu hiyo, kwani Cloud alikuwa na scene nyingi za kuigiza hata kuna wakati ambao Jack alikuwa anamwelekeza akimwambia siyo hivyo fanya hivi na Cloud kutii kama jina la muongozaji kaandikwa yeye itakuwa ajabu labda walisaidiana,”anasema Hidaya Njaidi
Bado wahusika wakuu wa habari hii, Jackson Kabirigi na Timoth Conrad wanatafutwa Ili kuweka sawa jambo hilo sambamba na mtayarishaji mkuu wa filamu hiyo maana siku hizi suala la Credit katika sinema linatumika vibaya.
source: filamucentral
No comments:
Post a Comment