Pages

Saturday, February 8, 2014

BODI YA FILAMU TANZANIA IMEPITILIZA KUHUSU SUALA LA MAADILI !

Dr.Cheni katika filamu ya Nimekubali Kuolewa amabyo imezuiliwa na bodi
Bishop Hiluka aliwahi kuandika kuwa tunahitaji BODI HURU YA FILAMU nchini tofauti na iliyopo sasa ambayo haipo huru na kama haijui kazi inayoifanya. Mimi nakubaliana kabisa na Hiluka kwa kuwa bodi hii haielweki kwa kuwa mara nyingi inalalamikiwa na wasanii kwa kuzuia kazi zao bila sababu za msingi kwa madai ya kulinda maadili ilihali kinachozungumziwa katika filamu husika ni kitu ambacho kipo katika jamii zetu na wakati mwingine hata filamu haihitaji kuzuiliwa but inazuiliwa kama ilivyotokea kwa filamu ya Dr. Cheni "Nimekubali Kuolewa" kwa madai  eti juu ya kava kavaa vazi la shera na kujipodoa sana !. kwa mujibu wa Dr.Cheni filamu hii inaonyesha madhara ya mapenzi ya jinsia moja(ushoga). Vipi kuhusu kina Joti katika Ze Comedy mbona bodi haiwapigi marufuku !. Ikumbukwe kuwa wakati ugonjwa wa UKIMWI ulipoingia duniani serilali ya Tanzania ilikuwa inasita kutoa elimu kuhusu ugonjwa huo mashuleni kwa madai ya kulinda maadili lakini vijana wengi walipoanza kupukutika kwa ugonjwa huo kwa kukosa elimu ya kujikinga ndipo serikali ikaamka na kuanza kutoa elimu mashuleni kuhusu ugonjwa huo.


Tuseme bodi ya filamu Tz haioni filamu za vitendo vya ngono kutoka nje ya nchi why zisipigwe marufuku kuingia nchini badala yake zimejaa sokoni huku bodi ikizuia kukua kwa tasnia ya filamu kwa kigezo cha maadili ! ni kweli maadili ni kitu muhimu lakini wengi wanakubali bodi ya filamu Tz imepitiliza kwa hayo maadili. Kwasasa ni vigumu wasanii kuigiza filamu inayoonyesha uozo wa viongozi wa juu nchini kwani bodi itazuia filamu kwa kigezo cha maadili. Kingine katika hivi vyombo/taasisi za kukuza tasnia ya filamu nchini wengine wamepewa uongozi wa kuongoza taasis husika ilihali hawajui nini maana ya filamu na sanaa kwa ujumla.

 Mfano katika filamu ya Nairobi Half Life(2012) kutoka nchini Kenya kulikuwa na tukio la mmoja wa wahusika wakuu(vijana wa kiume) kunyosheana  kidole cha kati kinachoashiria matusi ili kuleta uhalisia wa baadhi ya lugha za ishara zinazotumiwa na vijana hasa wa mtaani, filamu hii ni moja ya filamu chache nzuri zilizotengenezwa kwa lugha ya Kiswahili kiasi cha kupenya kwenye hatua ya awali katika tuzo za Oscars. Lakini kama hii filamu ingetengenezwa Tanzania ni lazima ingezuiliwa na Bodi ya filamu kwa tukio hilo la kunyosheana kidole cha kati kwa madai sio maadili na matokeo yake uhalisia kuondoka kama filamu zetu nyingi zilivyo. kama ni hivyo sasa hayo madaraja ya filamu huwa yanawekwa kwa ajili gani ! si waweke daraja moja tu linaloitwa "MAADILI" ili kila mtu ajue!

Kuna Professor mmoja wa chuo kikuu nchini aliwahi kuwa mmoja wa viongozi pale BASATA  siku moja nilimuuliza kwanini chuo unachofundisha wasanii wa filamu nchini wanasema hawaruhusiwi kurekodi hapa ilihali wewe ni mmoja wa viongozi wa idara ya sanaa chuoni hapa jibu lake lilikuwa "serikali haieleweki" hii ina maana kuwa hawa viongozi wakati mwingine wanakuta mfumo mbovu wa taasisi lakini wanashindwa kuubadilisha ni kama ilivyo hapo bodi ya filamu sasa kila kitu itakuwa ni kulinda maadili. Bikini kuvaliwa kwenye filamu ya kitanzania ni issue lakini katika video za muziki wa Bongofleva kuvaa bikini hakuna tatizo kabisa, hivi katika maadili kuna Tanzania 2! -yaani Tanzania ya filamu(yenye maadili) na Tanzania ya Bongofleva(isiyo na maadili kwa kuvaa bikini katika music videos), lakini mbona bikini ni vazi la ufukweni na hata kwa khanga au kitenge vyenye asili ya Afrika/tanzania vyaweza kutumika kushonea vazi hilo kwa msanii akiwa na scenes za beach !

Wasanii kibao wanalalamikia bodi kwa kuwa na longolongo katika makava ya filamu kuwa hayana maadili hata kama ni mpasuo tu wa gauni la msanii wa kike anatakiwa akapige picha ya kava upya.

Kwa ufupi ni kuwa mapenzi ya jinsi moja hayakubaliki katika jamii nyingi duniani kote, hata katika filamu za Bollywood suala hili halipewi uzito mkubwa kwa kigezo hicho cho cha maadili , filamu za Bollywood huonyesha suala la mapenzi ya jinsia moja ki-comedy zaidi kuliko katika filamu serious lakini wasanii mara nyingi huitwa na bodi na kukaa vizuri kufanya majadiliano ya pamoja ili kuweka kazi vizuri katika kupokelewa na jamii hasa katika kufikisha ujumbe. Tofauti na Hollywood ambapo filamu huwa jambo la kawaida kuonyesha mapenzi ya jinsia moja kwa kuwa jamii zao nyingine zimebariki kabisa suala hilo. Hivyo bodi ya filamu Tanzania ijitazame upya kwani imekuwa ikilalamikiwa sana kuwa inabana sana kazi za wasanii hata pale pasipo na tatizo kubwa badala ya kukuza tasnia ya filamu nchini bodi imekuwa ni moja ya vyombo vinavyolalamikiwa kuifanya tasnia ya filamu nchini isusuesue.


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

2 comments:

  1. BORA HIYO BODI WATUACHIE MADAKARAKA KWA WASANII ILI TUJIONGOZE WENYEWE

    ReplyDelete
  2. Bora sisi wasanii tungepewa madaraka ili tujiongoze wenyewe

    ReplyDelete