Pages

Saturday, January 11, 2014

PHOTOS: ACTRESS YUSTER NYAKACHAKA ATOA MSAADA WA VYANDARUA 400 NA KUANDAA CHAKULA CHA MCHANA KWA WATOTO YATIMA.

Muigizaji wa filamu nchini Yuster Nyakachaka ambaye filamu yake mpya akiwa na Jackline Wolper na Slim Omar inatarajiwa kutoka muda si mrefu ametoa msaada wa vitu mbalimbali  katika kituo cha watoto yatima na kina mama wajane wasiojiweza. Yuster muigizaji mwenye muonekano na umbo la kistaa alitembelea kituo hicho kitwaacho Madale Orphanage Centre kilichopo madale kata ya wazo. Muigizaji huyo aliandaa chakula cha mchana katika kituo hicho na pia kutoa vyandarau 400 kwa watoto na kina mama wajane waishio katika kituo hicho kama picha zinavyoonekana hapo chini. Muigizaji huyo pia alitoa vitu vidogo vidogo kama vile sabuni, mafuta ya kujipaka, nguo na viatu kwa watoto wote na pia khanga na vitenge. Angalia picha hapo chini.

Yuster aliyeshika mtoto akiwa na kina mama wa kituo hicho jana
Yuster akitoa msaada wa vitu mbalimbali jana katika kituo hicho

Wasanii wengine mliondekeza starehe bila kurudisha chochote kwa jamii inayosapoti kazi zenu igeni mfano.

Mungu akuzidishie sana Yuster kwa kuonyesha moyo wa kusaidia walio katika mazingira magumu.



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more

2 comments: