Friday, January 10, 2014

ACTRESS DEVOTHA ALFRED KUFANYA KAZI NA TWALEB ENTERTAINMENT.

Muigizaji Devotha Alfred ambaye ni mtanzania anayesoma nchini Ujerumani anatarajiwa kutokea katika filamu za Twaleb Entertainment ambapo kampuni hiyo inamilikiwa na mtanzania Abou Hermis Twaleb ambaye pia ni muigizaji na producer akiwa na makazi yake nchini Denmark kwasasa. Kupitia mtandao mmoja wa kijamii Abou aliandika "GOOD NEWS !!! ....ACTRESS DEVOTHA ALFRED NI MMOJA WAPO KATI YA WASANII WAKUBWA WALIOKUBALI NA KUWA TAYARI MDA WOWOTE
KUPIGA KAZI NA TWALEB ENTERTAINMENT MWAKA HUU 2014.....

TWALEB ENTERTAINMENT imeamua kuwataja wasanii wote watakaoweza kushiriki katika MOVIE zitakazofuata baada ya MOVIE YA KWANZA "AFRICAN BOY" KUTOKA......Sitopenda kuzungumza chochote kuhusu ni lini AFRICAN BOY ITATOKA.....ILA KAENI MKAO WA KULA KWA KUWA MWAKA HUU 2014 TE ITAWAPA KILE MLICHOKUWA MKIKISUBIRI KWA HAMU"


African Boy ndiyo filamu ya kwanza kutengenezwa na kampuni hiyo na mmoja wa waigizaji wakuu ni star wa filamu Swahiliwood, Lucy Komba.

Kila la kheri...............
                                                     Abou akiwa na Devotha

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news, life styles news and more.

No comments:

Post a Comment