Pages

Thursday, December 12, 2013

BAADA YA KUNYONYWA NA WASAMBAZAJI WA FILAMU KWA MUDA MREFU. MTITU AELEZEA MAFANIKIO YA 5 EFFECTS BAADA YA KUANZA KUSAMBAZA FILAMU ZAKE MWENYEWE.

William Mtitu ambaye ni mwigizaji, muongozaji na producer wa filamu Swahiliwood amefunguka kwa kusema kuwa awali ametumikishwa sana kwa kufanya kazi kubwa na kutoka jasho bila kuwa na faida ya moja kwa moja kwa kuuza filamu zake kwa wasambazaji ambao hutengeneza fedha na kujinufaisha wao badala ya watengena filamu.

Mtitu ambaye anamiliki kampuni ya utengenezaji na usambazaji wa filamu nchini ya 5 Effects amegundua hilo baada ya kuanza kutengeneza na kusambaza kazi zake mwenyewe bila kupeleka kwa wasambazaji ambao anasema ni wanyonyaji wasio na huruma kwa wasanii, halafu wanalalamika kuwa wanaibiwa lakini anashangaa hawaachi kusambaza filamu.

Akiongea na Filamucentral Mtitu ambaye ni mmoja wa wasanii wakongwe nchini alisema "Nawashauri wasanii na watayarishaji wenzangu wenye uwezo kusambaza kazi zao wenyewe badala ya kutegemea wasambaziwe na wasambazaji ambao hununua haki zao na kuwaacha maskini. badala ya kumjengea Mtitu chuki kwa mafanikio ya kupigana baada ya kudhulumiwa"
 
Mtitu amewashauri wasanii kuungana na kuanzisha kampuni yao ya usambazaji kwani yeye tayari amefanikiwa na kufanya utafiti baada ya kusambaza filamu zake ambazo ni Omega confusion na Nyati na kuona faida jinsi ilivyo kubwa hivyo kupata imani kuwa wasanii wakisambaza filamu zao wanapata faida kubwa kunufaika na kazi zao.

                                                                   Mtitu
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment