Pages

Thursday, December 5, 2013

MAINDA AMPAKA TENA LIVE JOHARI, RAY NA CHUCHU HANS NDANI.

Mainda
Uhusiano wa kimapenzi kati ya Vicent Kigosi(Ray) na Chuchu Hans bado upo kwenye mshike mshike mkali baada ya Mainda ambaye alikiri hivi karibuni Chuchu na Johari kumharibia penzi lake kwa Ray ameamua kumpaka live star mwenzake Blandina Chagula(Johari) kupitia mtandao mmoja wa kijamii baada ya hivi juzi Johari kuzungumza na gazeti moja la udaku na kusema kuwa Mainda amem-bip na yeye Johari atampigia. Kupitia Mtandao huo Mainda ambaye amejaaliwa kipaji kunako tasnia ya filamu ameandika...........

"...Hizi salamu zako Johari, ni hivi naomba usinitaje kwenye huo upumbavu wenu, Huyo mwanaume mnae mzungumzia mimi kwangu namuona mtu wa kawaida tu ndio maana nikamtupa kule. Nadhani umenipata halafu sitaki kumpandisha mtu jina sawa?. Ni hivi mimi si mpinzani wako, nadhani mpinzani wako unamjua mliopiganana (Sakata la Johari na Chuchu Hans kupigana)  mkataka kutoana roho kisa shingo ya kuku mlivyokuwa wajinga na malimbukeni wa mapenzi wanaume hawapiganiwi. Nimewakalia kimya naona wewe mwenye kilanga umejitoa kimasomaso ukaenda Kiu(gazeti) ukasema Mainda ame-bip wewe unataka kumpigia, ni hivi usiniweke kwenye upumbavu wenu, mimi huyo mwanaume wenu kwangu ni kuku kama kumtafuna nimemtafuna mpaka mifupa halafu nikatupa kwenye shimo la taka, sasa nyinyi mbwa koko mlio kosa wafugaji ndio mnaruka ovyo hamjui mle nini, pumbavu kabisa wewe na mke mwenzio si ndio hamkauki kunisema me mgonjwa, sasa kama me mgonjwa huyo bwana wenu ni hivi wewe mwenye shape kama ubao usiejielewa nakushauri achana na mimi nenda sinza…..(Itaendelea)"

                                               Johari


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

1 comment:

  1. where is NEY MACHAMGUDOA WAKO BONGO MOVE NIMEAMINI .WAMEGEUKA SAMAKI WALANA WAO KWA WAO SASA NGOJA KIMWI LIWAINGIE WATAPUKUTIKA KAA NZIGE ,MAANA HAPO WALIPO TAYARI WANAVIRUSI HII NI STORY YA BADO MIMI

    ReplyDelete