Friday, December 13, 2013

LULU NA YOUNG D WADAIWA KUFUMWA NDANI YA GARI WAKIFANYA MAPENZI.

Lulu na Young D
Juzi kupitia kwenye kipindi cha U-heard cha Clouds FM chini ya The Gossip Cop kulikuwa na tetesi kali zilizokuwa zinamhusu star wa filamu Swahiliwood Elizabeth Michael(Lulu) na mwimbaji wa muziki wa Bongofleva Young D. Wawili hao wanadaiwa kukutwa kwenye gari wakifanya mapenzi.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizo wawili hao walifumwa
na polisi wa doria wakivunja amri
ya sita maeneo ya Mbezi Beach ndani ya gari aina ya Hyundai inayomilikiwa na Lulu.

Habari zaidi zinasema baada ya wawili hao kukutwa eneo hilo na polisi walipelekwa pembeni gizani na kuongea na polisi kabla ya wao kutokomea kusipojulikana na gari hilo. Lulu alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu issue hiyo alipokea na kukata muda mfupi. Young D alipopigiwa simu alitoa majina ya utata kwenye kipindi hicho bila kueleweka vizuri.


                                                                     Lulu

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment