Liberty |
Hata kabla ya SWP kumuuliza Liberty kuhusu issue hiyo gazeti moja la GPL la leo likatoka na habari ambayo imemnukuu Ray akimtaja Liberty kama mpenzi wa zamani wa Chuchu kabla ya yeye(Ray) kutoka na Chuchu. "Niacheni na Chuchu wangu.... kifupi ndiye mke wangu na itawashangaza wengi. Halafu mimi nawashangaa sana. Yaani mimi kutoka na Chuchu mnakuzaaaa... mbona alivyokuwa na ma-boyfriend zake wengine hamkuandika? Kwa sababu ni Ray basi mkaona ni habari. Mimi ninavyojua Chuchu siyo mke wa mtu. kwanza mimi sijamchukua kutoka mikononi mwa mumewe(Frank Mtao) kama mnavyosema, Chuchu tayari alikuwa na maisha yake mapya, nilimchukua kutoka kwa Liberty, mbona alivyokuwa na huyo Liberty hamkuandika? kifupi niacheni na maisha yangu" alisema Ray akinukuliwa na Globalpublishers.
Liberty alipotafutwa na Swahiliworldplanet na kuelezwa kuhusu issue hiyo alionekana dhahiri kumshangaa Ray kwa kumzushia kutembea na Chuchu na Liberty alisema kuwa kamwe asingiweza kutembea na Chuchu ambaye ni mke wa rafiki yake Frank Mtao, aliongeza kwa kusema kuwa Ray ana roho mbaya na chanzo cha yote hayo ni filamu yake ya Laura aliyocheza na Chuchu ambayo hata bado haijatoka na Chuchu alipomuonyesha Ray hiyo filamu na kuiona ni nzuri ndiyo akaona atembee na Chuchu akidhani kuwa Liberty na Chuchu ni wapenzi ili amharibie Liberty kumbe sivyo kwani yeye(Liberty) hajawahi hata siku moja kutembea na msanii wa filamu nchini. "Duuh sio kweli sikuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Chuchu nilimheshimu kama mke wa mshikaji wangu Frank Mtao wala sikuwahi kufikiria hilo"
Liberty aliongeza kwa kusema " Ila ni story ndefu ni wivu wa kazi ndiyo umemfanya mpaka Ray kamsaliti rafiki yake Frank kwa kuhisi ananikomoa mimi na tatizo ni ile movie ya Laura ni movie kali sana Chuchu alivyomuonyesha bwana wake Ray roho mbaya na wivu wa kutotaka watu wafanye kazi nzuri ndiyo tatizo. Hawa wasanii wakubwa ukimtoa Richie(Single Mtambalike na Cloud wengine wote wana roho dhaifu sana wakiongozwa na mwenyekiti wao Ray. Daah jamaa wana roho mbaya sana kuliko sana wanatamani tasnia hii iwe yao peke yao wakiona mtu unafanya vizuri baada ya kukusaport wanakupiga vita wakupoteze sasa hawajui mimi nafanya movie 4 fun sio natafuta maisha au hela ya kula. Hakuna msanii hata mmoja Bongo mwenye hata robo ya mali zangu wakienda China wanahisi wamemaliza wakati mwenzao nataka kuimaliza dunia naishi Uk nafanya kutembea tuu bongo"
"Duu nimesikitika sana kuliko sana Ray anasema amemtoa Chuchu kwangu na sio kwa mumewe duuh sasa Ray na Frank si marafiki au anataka umaarufu na kuharibiana majina!, kama kuna mwanamke yeyote wa Bongo movie aliwahi kutembea na mimi ajitokeze nitampa chochote anachotaka mimi najitambua kuliko sana siwezi kutoka na watu ambao mnafanya nao kazi me na cheap girls wapi na wapi no time daah jamaa kanikwaza kinoma" alimalizia Liberty
Ray na Chuchu Hans
No comments:
Post a Comment