Pages

Thursday, December 12, 2013

HII NDIYO MAHARI ANAYOITAKA LULU KWA MWANAUME ANAYETAKA KUMUOA.

Mwanaume atakayetaka kumuoa Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni star mkubwa wa filamu Swahiliwood atalazimika kutoa si chini ya shilingi laki nane (800,000) kama mahari ili kumuoa star huyo.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichozungumza na Globalpublishers wanaume wengi wamekuwa wakimendea kufunga ndoa na Lulu lakini wanashindwa njia za kumpata.
Inadaiwa kuwa kikwazo kikubwa wanachokutana nacho ni namna ya kumfikia na kigezo cha dini kwa sababu Lulu hataki kuolewa na muislam kwani hayupo tayari kubadili dini.

Akizungumza na Globalpublishers mama wa Lulu, Lucresia Karugila alisema kwa upande wake yupo tayari kupokea mahari yoyote ilimradi mwanaye awe ameridhiana na mwanaume husika. "Unajua Lulu ameshakua, mambo ya kumwingilia mtoto kwenye vitu binafsi ni ya kizamani"
"Siwezi kupanga mahari, sijui laki nane au laki ngapi. Kiasi chochote ni sawa cha msingi mwanangu awe amekubaliana na huyo mwanaume, hajaniambia kama kuna mtu anataka kuleta mahari" alisema mama Lulu

Kwa upande wake Lulu alisema "Kwa sasa sina wazo la kuolewa ila naweza kuamka kesho nikabadili uamuzi". Alipoulizwa na mtandao huo kama ni kweli atatakiwa kulipiwa mahari ya laki nane alisita kidogo.
Kuhusu kigezo cha dini star huyo wa Swahiliwood alikiri kuwa kati ya vitu anavyozingatia ni hicho kwani hataki mwanaume wa kumbadilisha dini na mahari yake itategemea na mtoaji .

                                                                        Lulu


Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

1 comment: