Devotha |
SWP: mzima Devotha? wewe ni mtanzania au? and unakaa germany au Denmark?
DEVOTHA: Mzima sijui we we.mi ni mtanzania naishi Germany ila Denmark naenda kufanya film tu
SWP: Ulianza lini sanaa ya filamu and huko Germany unasoma au umeolewa?
DEVOTHA: Sanaa nilianza mwaka .2011 nilicheza kwenye movie ya Misukosuko, Ndoa Ya Utata na Daktari Wa Giza .Tanzania nimesomea films chuo kikuu Mlimani(University of Dar es salaam), Germany nasoma. Jina langu kamili ni Rosemary Alfred Mahali ila natumia Devotha sana ni jina langu la utotoni.
SWP: Now unasoma huko una mpango wa kurudi Tanzania au ndiyo wataka kufanya mishe za kwenda Hollywood kabisa?
DEVOTHA: Mipango ya kwenda Hollywood ipo na hata sasa kuna kampuni ndogo ndogo za marekani zinanitaka kufanya nao Kazi .sehemu mbalimali ila shule inabana kusafiri mbali .Na Tanzania ni nyumbani ntarudi tu hakukwepeki pia Nina mipango ya kufanya fillm na mastaa wa Tanzania na nchi mbalimbali za kiafrika .ila kwa sasa bado nipo shule, pia nataka nifanye films nyinyi za kuwaonyesha waafrika maisha ya huku ulaya maaana tunajua mambo mengi ya Africa kupitia movies za kiafrika.sasa ni muda wa kuwaonyesha waaafrica maisha ya ulaya huku tukitangaza lugha ya kiswahili.
SWP: Umefanya filamu ngapi huko Ulaya mpaka sasa?
DEVOTHA:
Huku Europe nimefanya movie mbili ya kwanza short film passport love ambayo Mimi ndio mwandishi Na ya pili ndio hio bado jina halijawekwa wazi Vad Production tuliofanya Na Mr nice.
Picha chini inamuonyesha Devotha akiwa behind the scenes ya filamu ya Passport Love
Keep it up girl
ReplyDelete