Pages

Thursday, November 28, 2013

RAY NA JOHARI WANA LAANA YANGU: NORA

Nora

Baada ya hivi karibuni staa wa filamu nchini Ruth Suka(Mainda) kueleza mazito kuhusu Vicent Kigosi(Ray), Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao.
Akizungumza na Globalpublishers Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni.

"Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na kidole."alisema Nora aliyewika sana miaka ya nyuma

Muigizaji huyo aliyejaaliwa mvuto na kipaji aliongeza kwa kusema "Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye atamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza kwenye fani.
Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa, mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui zangu wote wataumbuka mchana kweupe"

Mtandao huo  uliposhindwa kumpata Ray kwa kumpigia simu ulimtumia ujumbe ambapo alijibu kwa kifupi."Dah, kiukweli kama Nora ndiye kasema hivyo basi mimi sina comment yoyote na madai hayo na kirahisi naomba uandike hivyohivyo"

Kwa upande wa  Johari alipotumiwa ujumbe kuhusu issue hiyo hakujibu.

                                                                      Ray

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

2 comments:

  1. @ NORA, USIHUKUMU ILI NAWEWE USIJE UKAHUKUMIWA. ULISHA VUNJA AMRI YA MWENYEZI MUNGU. KWAHIYO NAWEWE UKUMU YAKO INAKULENGA. SORRY! Ramsey USA.

    ReplyDelete
  2. mbonaa nora tunakujua kama nora na Johari kama johari? na hata ktk dangerous desire tumekuona ukicheza na johari....wasanii acheni mneno Industry haitafika popote angalieni wenzetu GHana, nigeria wapo wapi sasa hv.... mimi naona hujapotea kabisa wewe fanya kazi kwa bidiii tutakuona na tutanunua kanda zako

    ReplyDelete