Pages

Thursday, November 28, 2013

INTERVIEW WITH SELEMBE TOKO: NASUMBULIWA SANA NA MADEMU, JACKLINE WOLPER, LUCY KOMBA NAWAKUBALI SANA.

Selembe
Selembe Toko ni muigizaji wa filamu za Kiswahili nchini Denmark ambaye ameanza kukubalika kwa mashabiki. Muigizaji huyo tayari alishaigiza filamu moja na Lucy Komba filamu ya Tanzania To Denmark. Swahiliworldplanet ilipata nafasi ya kuzungumza nae kuhusiana na kazi zake za filamu na maisha binafsi kwa hiyo shuka nayo hapo chini........................

SWP: Unayaonaje mazingira ya filamu za kiswahili Denmark na Scandinavia kwa ujmla wewe kama msanii?

SELEMBE: kwasasa naona mambo yanaendelea vizuri lakini hawana mawasiliano, hakuna umoja wa dhati kila mtu anajipendelea mwenyewe na wasanii wengine unakuta wana wivu.

SWP: Vipi kuhusu kisanii unazidi kukua tangu ulipocheza filamu yako ya kwanza?

SELEMBE:  Ndiyo nakuwa zaidi sababu watu wanafurahia kazi zangu nilizocheza Norway na pia nimealikwa tena kwenda Holland kucheza filamu mwezi December na Sallai Majasiri ambaye ni muigizaji wa huko na alikuwa hapo Tanzania, anafanya filamu kwa kazi za injili na filamu yake mpya inaitwa Mwanzo Mwisho.

SWP: Una mke na watoto au mchumba?

SELEMBE: Sina mke wala mchumba ila nina mpenzi ambaye bado namchunguza kwanza tabia muda wa uchumba ukifika nitawajulisha.

SWP: Unafikiri nini kinahitajika zaidi ili filamu za kiswahili zinazotengenezwa nje ya Afrika(scandinavia) zifike mbali zaidi?

SELEMBE:  Inahitajika maelewano na watu vizuri na kufanya kazi kwa bidii.

SWP: Ni changamoto gani umekumbana nazo katika kazi zako za sanaa?

SELEMBE: Filamu zilizonipa changamoto wakati wa kushuti ni Jealous Friend na Moyo Wangu na ndiyo ambazo nazipenda sana siku hizi.

SWP: Katika waigizaji wa filamu za kiswahili huko Scandinavia unamkubali zaidi msanii gani?

SELEMBE: Katika filamu hapo Scadinavia nawakubali wasanii kama Papi Zongwe,  Tatu Daniel,  Zawadi Justine, Magie Seluwa, Sallai Fataki na Blandine Julber Fataki.

SWP:  Lucy Komba ambaye ni star mkubwa wa filamu Tanzania na aliyeibua mastaa wengi wa filamu huku amewahi kukiri kuwa una kipaji na kama utaendelea na nguvu hiyo hiyo utafika mbali, je walizungumziaje hilo ukifikiria pia kuwa umecheza naye filamu ya Tanzania To Denmark?

SELEMBE: 
kwakweli hiyo movie watu wanaikubali na wanaisubiria kwa hamu kubwa, tena Lucy komba watu wana mkubali sana huku Ulaya sababu anajuwa tena ana akili ya kufanya movie nzuri, Tanzania To Denamrk ndiyo filamu iliyonipandisha zaidi tena ilikuwa ndiyo mara yangu ya kwanza kucheza movie na msanii mkubwa kama Lucy, tena alifurahi sana na kunipa moyo ili niendelee na uigizaji.

SWP: Kwa hiyo ungependa siku za baadaye ucheze nae tena filamu mkiwa nyie ndiyo wahusika wakuu?

SELEMBE: Ndiyo na  hivi tunasubiria Tanzania To Denmark itakuwa sokoni muda si mrefu.

SWP:  Hupati usumbufu kutoka kwa mademu/wanawake baada ya kuanza kuwa maarufu?

SELEMBE:  Tena sana nasumbuliwa saaana tena usiku sawa mchana.

SWP: Pole, kwa hiyo huwa unawakubalia au?

SELEMBE:  Hapana, tena hivi nabadilisha number ya simu kila siku.

SWP: Hufikirii kuwa hiyo ni nyota ya mvuto na kazi zako zinakubalika !

SELEMBE:  Ndiyo lakini ni majaribu tena kwa mchumba wa mtu, ukiwa na mke au mchumba itakuwa vurugu kila siku ha ha ha haaaa.

SWP: Ni muigizaji gani wa kiafrika unamkubali sana kikazi?

SELEMBE:  Lucy Komba, Mercy Johnson, Jackline Wolper, Aunty Ezekiel na Vicent Kigosi(Ray)
.
SWP:  Media za huko Denmark na Scandinavia huwa zinamipa ushirikiano mzuri katika kazi zenu za filamu?

SELEMBE: Siyo sana.

SWP:  Ungependa kuwaambia nini wasanii wenzako wa filamu wa huko Scandinavia na mashabiki wako kwa ujumla?

SELEMBE: ningependa kuwambia mashabiki wangu nawapenda saaaana na wazidi kunisapoti, na wasanii wenzangu tupendane na tusaidiane kikazi na tuache wivu.

Selembe Toko kulia akiwa katika moja ya shooting ya filamu alizocheza



Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment