Pages

Sunday, November 24, 2013

NI KAWAIDA KUPATA USUMBUFU KUTOKA KWA MADEMU LAKINI NAWAELEZA UKWELI ILI WANIHESHIMU: WALTER DE NGONDE.

Walter
Walter De Ngonde ambaye ni star wa filamu nchini anayekuja juu kwa kasi amesema kuwa yeye kama kijana anapata usumbufu kutoka kwa mademu lakini anachofanya ili mademu hao wamheshimu ni kuwaeleza ukweli tu kuwa tayari anaye mtu wake ambaye wanapendana. Walter ambaye anakuja na filamu mbili mpya za V.I.P na Love Maniac kutoka RJ Company ambazo yupo na Vicent Kigosi(Ray), Jackline Wolper, Chuchu Hans na waigizaji wenginene wenye majina aliyasema hayo alipoulizwa na Swahiliworldplanet kuwa hapati usumbufu kutoka kwa mademu baada ya jina lake kuanza kuja juu na muigizaji huyo ambaye pia ni model aliyetokea kwenye matangazo kadhaa ya Tv na billboard alisema "Nalichukulia ni jambo la kawaida,wapo wanao nisumbua ila ili kuwafanya wakuheshimu ni kwa kuwaambia ukweli tu"

Ukiachilia mbali filamu hizo kutoka RJ Company Walter tayari amecheza filamu nyingine akiwa na Irene Uwoya na nyingine mpya ya Coast To Coast akiwa na Slim Omar na Yobnesh Yusuph(Batuli). Walter ana mtoto mmoja wa kiume.

                                                                 Walter

 
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

2 comments:

  1. huyu mkaka yupo sexy sana i wish siku moja anikumbatie, kina chuchu na Johari watakuwa wanammezea mate hapo RJ

    ReplyDelete
  2. Chuchu na johari c wamekufa ngozi?

    ReplyDelete