Pages

Wednesday, November 20, 2013

MWANAMUZIKI AY AMUANIKA HADHARANI MCHUMBA WAKE MWENYE ASILI YA YEMEN NA SHELISHELI.

AY ni msanii maarufu wa muziki mpaka nje ya Afrika mashariki na kati akiwa anatokea nchini Tanzania ila mashabiki wake wengi hawamjui mchumba wake licha ya kwamba wanaweza kuwa baadhi yao walishawahi kuwaona wakiwa pamoja. Huyo hapo chini ndiye mpenzi/mchumba wa AY na ana asili ya Yemen na visiwa vya Shelisheli. Hapo ilikuwa Jumapili iliyopita Club Bilicanas katika show ya AY iliyopewa jina la Road To CHOAMVA 2013. Ay ambaye yupo katika mipango ya kuoana na mchumba wake huyo amesema katika harusi yake hatachangisha michango kama baadhi ya wasanii au watu wanavyofanya.

Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

No comments:

Post a Comment