Pages

Saturday, November 23, 2013

LULU AMPOTEZEA DIAMOND KIMAPENZI LICHA YA KUAHIDIWA GARI LA ZAIDI YA MILIONI 60.

Lulu
Elizabeth Michael(Lulu) ambaye ni star mkubwa wa filamu Swahiliwood anadaiwa kumpotezea Diamond Platinumz anayehaha kutaka ku-enjoy penzi lake kiasi cha kufikia kutaka kumnunulia Lulu gari aina ya Nissan Murrano yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 za kitanzania lakini Lulu amechomoa na kudaiwa kubadilisha namba ya simu ili asipate usumbufu kutoka kwa Diamond Platinumz.

Habari zaidi ambazo zimeripotiwa na gazeti moja na mitandao kadhaa zinazidi kusema kuwa moja ya lengo la Diamond kutaka penzi la Lulu ni kutaka kuzidi kutawala vyombo vya habari kwani Lulu ni star mkubwa na mwenye mvuto kwenye media na mashabiki wengi pia anao hivyo akiwa nae kimapenzi umaarufu wake utazidi kuongezeka maradufu kwa kutawala media kila siku lakini Lulu hasikii la muadhini wa la mnadi swala katika hilo na hivi majuzi tu Lulu alitangaza kumzimikia Justin Bieber ili kuzidi kumvunja moyo Diamond ambaye ametoka na mastaa kadhaa kama vile Wema Sepetu, Jackline Wolper, Peniel Mungilwa, Rehema Fabian, Jokate na wengineo na wasichana wengi bado wanaliwinda penzi la Diamond.

Mpaka sasa watu wanajiuliza ni mwanaume gani huyo anayempa jeuri Lulu kiasi cha kumuona Diamond si kitu mpaka kubadilisha namba ya simu.

                                                           Diamond Platiunumz
Follow us on twitter Swahili World Planet  and Like our facebook pages Swahili World Planet and Bongomovies SWP for more updates about Swahili movies latest news, gossip, celebrities, features, beauty, fashions, music plus Hollywood, Bollywood and Nollywood news.

2 comments:

  1. endeleeni kupost mambo ya mastaa huku wanafunzi wa kitanzania wanaosoma msumbiji wanakufa njaa na blog/ media zote zinashindwa even saidia kupost habari zao eti kisa sio masupastaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. blogs zinaweka habari kutokana na kupatikana kwa habri hizo na kama bloggers hawana taarifa hizo wataziwekaje ukifikiria ni habari kutoka nchini nyingine, blohs zote haziwezi kuweka habari za aina moja na zipo nyingi tu zinazoweka haabri za kijamii kama hizo, sisi tunadeal zaidi na habari za entertainment lakini kwa kuwa ni habari muhimu wewe mwenye taarifa nazo tupe kupitia email hii swahiliworldent@gmail.com and tutaweka na bloggers wengine pia wataziona na kuweka. ahsante pia kwa comment yako

      Delete